Mwanangu usitembee na mume wa mtu

Mwanangu usitembee na mume wa mtu

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
MWANANGU USITEMBEE NA MUME WA MTU ..

Binti mmoja alikua anatembea na mume wa mtu, alikua akifanya kwa siri lakini Mama yake alijua, baada ya kuona vile Mama yake alimkalisha chini na kumuuliza kwanini anafanya vile? Binti hakua na jibu la maana lakini alimuambia Mama yake yeye anamheshimu mke wa huyo jamaa na hawezi kumvunjia heshima. Alimuambia anafanya kimya kimya na kamwe hawezi kumuumiza kwani hatajua.

Mama yake alimuambia kuwa ipo siku atajua na ataumia, binti hakumuelewa, alimfuata jamaa yake na kumuambia kuwa awe makini mke wake asijue kwani akijua atamuumiza, alimuambia amheshimu mke wake, awe anafuta meseji zake na ikiwezekana watafute laini nyingine kwaajili ya mawasiliano. Mwanaume kweli alitii na walifanya kimya kimya lakini Mama bado aligundua na kujua mwanae anaharibu ndoa ya watu.

Yule binti alikua anapewa pesa nyingi na anazipeleka benki, kila siku akipewa alikua anapeleka benki. Baada ya mwaka mmoja binti alitaka kuzitumia pesa zake, lakini alipofika benki alikuta pesa zote zimechukuliwa. Binti alishangaa na kuanza kuhangaika, aliwauliza watu wa benki wakamuambia zimetolewa na kadi yake kwenye ATM, aliulizwa kama aliwahi kuipoteza akasema hapana, waliangalia katika Camera na kuona picha za mtu anayetoa pesa zake.

Alikua ni Mama yake, Benki waliuliza kama anamfahamu alisema ndiyo ni Mama yake hivyo hawezi kumshitaki. Alitoka akiwa na huzuni, kurudi nyumbani alimuuliza Mama yake kwanini alikua anachukua pesa zake. Mama yake alimuambia “Niliiona ATM Card yako nikajua na Password yako hivyo nikaamua kuzichukua kimya kimya nikijua kwamba hutaumia kwani nakuheshimu wakati wakuchukua sikuambii na sizitumii mbele yako.

Ningekua nazichukua nakufanyia starehe mbele yako ungeumia ndiyo maana nikachukua kimya kimya.” Mama alimaliza kuongea na kuondoka, binti alibaki analia kwani zilikua pesa nyingi sana na asingeweza kumfanya kitu chochote Mama yake. Aliamua kutulia tu, baada ya siku mbili Mama yake alimletea zile pesa na kumkabidhi, binti alishangaa na kumuuliza kwanini alizichukua na kwanini amezirudisha, Mama yake alimuambia;

“Nilitaka nikuonyeshe kwamba mtu anapokuibia kitu chako hata kama ni kimya kimya kuna maumivu. Hutaumia wakati anaiba kwani hutajua lakini siku ukija kujua basi utaumia mwizi ni mwizi tu awe amekuibia kwa kukukwapulia mtaani au kwa kuiba benki kidogo kidogo ipo siku utajua na maumivu yake ni yaleyale. Wewe ni mwizi unaiba mume wa mtu mkewe anaweza asiumie sasa kwakua hajui ila sikua kijua ataumia kama vile ndiyo unamuiba sasa.”

Mama alimaliza kuongea, binti ambaye alishaanza kujisikia vizuri kwakua hatembei na mume wa mtu waziwazi alianza kujisikia vibaya na siku iliyofuata aliachana na yule mwanaume. Alianza kujihisi vibaya kwani siku zote alikua akijipa moyo kuwa kwakua mkewe hajui basi hafanyi kosa lakini alianza kuwa na wasiwasi kuwa ipo siku mkewe atakuja kujua na maumivu yake hayatakua na tofauti na yale ambayo angeyapata kama angefanya kwa wazi hivyo akamuacha yule mwanaume.

MWISHO; Kama unafanya fanya tu lakini si kujishaua eti “Mimi nafanya kimya kimya”
 
''Kama unafanya fanya ila sio kujishaua kuwa nafanya kimya kimya''
 
Ujinga ujinga tu. Binti muache apoze roho ya mwanaume, kwenye ndoa kuna stress
 
Back
Top Bottom