Kwema,
Sisi vijana tusio na ujuzi zaidi ya kile tulichosomea ni tabu sana huku mtaani.
Mtu unamaliza chuo bila ujuzi wa ziada wa kukusaidia kitaa aloo ndo maana tunasota sana.
Wazazi msiwatumie watoto wenu kwenye shughuli zenu za kukuza kipato chenu, walau hata muwapeleke mahali kama veta wakajifunze fani yoyote. Ni bora awe anaacha kitu mezani kuliko kumshindisha kwenye biashara/kilimo au mifugo yako ambako mara nyingi huo ujuzi anaoupata kuuapply ni mpaka awe na mtaji.
Mtoto wa kike mpeleke ajifunze ushinonaji, kupika keki, mapambo hata akienda advance anakua na kibunda.
Bora hata hao wanaowashindisha kwenye biashara zao, kuna hawa wa kusubiri matokeo. Yaani mtoto kachill tu kucheza game, kuangalia tv mpaka matokeo yatoke wajue anaenda wapi ndio wapanga afanye nini, akifeli bado watamkomalia arudie shule wakati fursa mtaani ni nyingi tu..
Kuna dada mmoja alimaliza na bahati mbaya hakua na ufaulu mzuri. Mzee wake akampeleka advance kwa lazima nako huko akafeli( kwenye mchujo shuleni kwao), akarudishwa nyumbani.
Mzee wake akapanga tena amrudishe shule lakini kabla ya hapo akampeleka kujifunza ufundi cherehani, sasa hivi ni fundi mzuri tu na wala hawazi shule ila kuikuza biashara yake zaidi.
Haya mambo ya kulazimisha shule huwa yanawacost sana wazazi, ile likizo ndefu ya form 4 ndio kipindi cha kumjua mwanao ni mzuri kwenye fani gani.
Ile miezi mingi isiende bure tu, tuwaandalie mazingira hawa vijana. Sometimes ile spirit ya upambanaji inatengenezwa mtu hazaliwi nayo, ukimzoesha mwanao kua akufanyie kazi wewe tu kwa kutulmia akili yako tu ni lini sasa utamfunza kutumia yake?
Watoto wa kike wanajiuza wakimaliza vyuo kwasababu kurudi nyumbani hataki, akibaki ajitegemee ndo hivo hana ujuzi wowote kitaa na anatakiwa apate pesa ya kula na nauli, afanyaje?? Na anaogopa kurudi home kua mzigo maana haingizi chochote nyumbani zaid ya haja uani tu!! Anaona aibu.. si ajabu huyu angekua na ujuzi angerudi nyumbani kuuendeleza tu.
Muandae mwanao, dunia imeharibika hii. Usiseme mimi sikuandaliwa hivyo nae ajiandae mwenyewe. Usipomuandaa wewe ataandaliwa na walimwengu..
Alamsiki.