Mwanariadha Alphonce Felix Simbu Ashinda Medali ya Shaba, Daegu Marathon Korea Kusini

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414


Mwanariadha wa Kimataifa wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu ashinda medali ya Shaba kwa kushika nafasi ya Tatu , kwa muda wa (2:07:55) kwenye Mashindano ya DAEGU MARATHON yaliyofanyika usiku wa leo 7/04/2024 huko Korea Kusini.

Mshindi alikuwa Stephen Kiprop ; 2:07:04 na pili alikuwa Kennedy mutai ; 2:07:40 na tatu Alphonce Simbu ; 2:07:55.
 
Hii ni habari njema sana kwa Taifa la Tanzania hasa wizara ya michezo kwa ujumla.

HONGERA SANA ALPHONCE FELIX SIMBU.

Sema ndio hivyo tuna selikali ya Ajabu ambayo imekikita zaidi kwenye propaganda imeamua kiwageka waganzania Kupitia simba na Yanga.

Watanzania wanachokiwaza wao ni simba na yanga.
Wizara haina habari na Riadha wao ni simba na Yanga Tu.

Nji yetu masikini tunashindwa hata kuhamasisha michezo mingine ni simba na Yanga tu.

Ukiingia hapa Jf ni kujaza seva ni simba na Yanga tu
 
Tuendelee kujifunza, na kuwabadilisha watu Fikra zao, zihamie Kwenye Riadha.

Kwa mfano; mshindi wa dhahabu Olimpiki anachukua milioni 125
 
Hongera Sana ndugu Alphonce Felix Simba 🦁
 
Huu mchezo na ndondi ndo michezo pekee iliyowahi kuiletea Tanzania heshima. Nampongeza sana Alphonce kwa kupata medali. Huyu kijana aliingia Arusha kutokea kwao Singida akiwa mdogo sana kiumri na hakuonekana kabisa kama ana kipaji cha kutosha. Nakumbuka kuna mkongwe mmoja alimshauri aache kufosi riadha na ajikite zaidi na shule. Dogo alijitahidi kumaliza kidato cha nne huku akiendelea kujifua. Hata baada ya kumaliza shule ilimbidi apige tena tizi kali kwa miaka kama mitatu ndo akaanza kuwika. Kwa sasa Alphonce ni tajiri. Nikiwachukua wanamichezo na wasanii wote atakuwa kapitwa na wachache sana kwenye suala zima la pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…