Mwanariadha Alphonce Simbu awasili nchini na Medali ya Shaba kutoka Korea Kusini

Mwanariadha Alphonce Simbu awasili nchini na Medali ya Shaba kutoka Korea Kusini

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
3ec91505-0839-49b7-add8-82262e1bf1bc.jpeg

Mwanariadha wa Kimataifa wa Tanzania toka (JWTZ) Sgt. Alphonce Felix Simbu awasili Tanzania Kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupokelewa na Viongozi wa Michezo na Makocha kutoka Jeshi la ulinzi la wananchi la Tanzania (JWTZ) baada ya kushinda kwa kushika Nafasi ya Tatu na kushinda Medali ya Shaba Kwa Muda wa 2:07:55 kwenye Mbio za DAEGU MARATHON 2024, huko Korea Kusini.

Wakati huo huo, Alphonce Felix Simbu Ametua nchini tayari kwa maandalizi ya kushiriki mashindano makubwa ya Olimpiki yatakayofanyika Paris Ufaransa Julai 26 hadi Agusti 11, 2024, mashindano ambayo mshindi wa kwanza wa medali ya Dhahabu atajishindia kitita cha zaidi shilingi milioni 125 za Kitanzania ( US $50,000), atashiriki mashindano hayo pamoja na wenzake waliofuzu ambao ni Gabriel Gerald Geay, Magdalena Shauri na Jackline Sakilu.
 
Hongera sana. Naamini hayo mashindano ya Ufaransa atafanya vema zaidi na kushinda hicho kitita.
 
Back
Top Bottom