Mwanariadha Gabriel Gerald Geay atua Sydney Australia kushiriki mbio za Sydney Marathon Jumapili ijayo

Mwanariadha Gabriel Gerald Geay atua Sydney Australia kushiriki mbio za Sydney Marathon Jumapili ijayo

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
IMG_3646.jpeg
Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania Gabriel Gerald Geay atua jijini Sydney Australia kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa ya Sydney Marathon tarehe 17 septemba 2023 jumapili.

Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha wanariadha zaidi ya elfu arobaini (40,000) wanaotoka katika nchi 66 duniani.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanzia , Bradfield Park, milsons point na kumalizikia Sydney Opera House Forecourt huko Sydney Australia.

Gabriel anakwenda akiwa na muda mzuri wa 2:03:00 kwa mbio za marathon, yaani kilomita 42.195 na akifanya vizuri zaidi itamuweka sehemu bora zaidi.

Pia, kwenye mbio hizi anatarajia kupata donge nono kutoka kwenye kampuni yake (Adidas), kupitia meneja wake.
 
🤣🤣🤣Hawa Watanzania wa kuwaza Simba na yanga hawawezi msapot
Labda angekuwa Max zengeli
Wazee wa kufata upepo
Kizazi Cha vilaza🤣🤣
 
🤣🤣🤣Hawa Watanzania wa kuwaza Simba na yanga hawawezi msapot
Labda angekuwa Max zengeli
Wazee wa kufata upepo
Kizazi Cha vilaza🤣🤣
Tunaendelea kuwawekea vichwani mwao Riadha ni mchezo mkubwa na wenye pesa nyingi sana
 
HABARI ZENU...SYDNEY MARATHON TUMEMUONA OTHMANE EL GOUMRI AKICHUKUA GOLD, TUNAOMBA MTUJULISHE NINI KIMEMKUTA GABRIEL GEAY MAANA KAMA SIKOSEI AMEPOTELEA NJIANI WANAUME WAKAGONGA PACE...
Ameshindwa kumaliza, after 35K
 
Geay kushiriki Valencia marathon leo 3 Dec. Mungu ibariki Tanzania.
  • The race will be available on Kenya SuperSport, KBC, StarTimes, KTN, NTV, and Canal+.
Start time 10.15 AM .
 
Back
Top Bottom