Mwanasheria Mkuu amuonya Raila kushtakiwa kwa uhaini endapo atajiapisha

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Githu Muigai ameonya kuwa Raila Odinga akijaribu kujiapisha tarehe 12 kama alivyopanga atashtakiwa kwa kosa ya uhaini ambalo adhabu yake ni kifo

Amesema kuapishwa huko kutakuwa ni kinyume cha Katiba ya Kenya kwa sababu tayari kuna Rais aliyekwisha apishwa Novemba 28.

Kumuapisha mtu yeyeote ambaye hajatangazwa tume ya uchaguzi kuwa ameshinda uchaguzi na ambao hajasimiwa na Jaji Mkuu ni kinyume na Katiba na Uhaini wa hali ya juu



Pia mwanasheria huyo ameonya Kaunti 11 zilizopitisha mjadala wa Bunge la Watu na kusema wamevunja sheria na wanatumia vibaya pesa za walipa kodi




Wakati huo huo Raila Odinga amepuuzia wito wa Marekani wa kumtaka asijiapishe na kusema masuala ya Kenya yatasuluhishwa na Wakenya wenyewe

Ameendelea kusema wanaweza kuwashauri lakini sio kuwaambia kuwa wanavunja katiba

Na kusema watu walipokuwa wanauawa na polisi hakuna balozi aliyejitokeza kulaani mauaji hayo
=============================================

Attorney General Githu Muigai has said that the controversial swearing in of opposition leader Raila Odinga slated for Tuesday, December 12 amounts to high treason.

Speaking at Sheria House on Thursday, the AG warned that persons that will facilitate or be involved in the event will face the full wrath of the law.

“The constitution of Kenya provides in clear terms in Article 2 (2) that no person may claim state authority except as authorised by the constitution. A swearing-in of any other person not declared to have lawfully won an election by IEBC and administered by the Chief Justice is high treason in respect of the person involved and any other facilitating that process,” said the AG

Muigai cited the Constitution which prescribes death as the punishment for treason.

“What is the punishment for high treason? It is death,” he said.

He also dismissed claims by the National Super Alliance (NASA) that formation of the People’s Assemblies is legal.

“The People’s Assembly is an institution totally unknown to the constitution of Kenya and totally unknown to the County Governments Act. Parliament has not delegated any such power and the consequence for that is that those institutions are unconstitutional,illegal and are null and void,” said the Attorney General.

He added that counties that have passed the People’s Assembly motion should be ready to be held to account.

Source: Citizen Tv
 
What is the punishment for high treason? Death. Wamuapishe huyo mshenzi tuone next move yao kama haitakuwa ni mazishi.
 
What is the punishment for high treason? Death. Wamuapishe huyo mshenzi tuone next move yao kama haitakuwa ni mazishi.
Patanuka lakini na watu kuuawa tena, huyu jamaa yenu sijui vipi anakosa busara kiasi hiki
 
Patanuka lakini na watu kuuawa tena, huyu jamaa yenu sijui vipi anakosa busara kiasi hiki
Raila mwenyewe anajua hilo na ndo nia yake kuu. Vifo huwa vinamuinua sana kisiasa. Nawahurumia wafuasi wa NASA wanamfata huyu jamaa kama vipofu,wakati wanajua vyema ni mtu wa aina gani.
 
Akikumbuka makafara aliyofanya hadi kumtoa Fidel bado urais hajapata anaona bora watu wafe
 
Mambo ya katiba mpya hayo[emoji1321][emoji1321][emoji1321]
Na faida za demokrasia[emoji1321][emoji1321]
Baba Jeska chapa kazi baba
Ipo siku watakuelewa tu,,na watajiona wajinga
 
Sijaona point ya Raila kujiapisha:-
(1.)Uchaguzi wa kwanza alienda Mahakamani, na Mahakama ika ufuta na kuitisha uchaguzi mwingine.
(2.)Uchaguzi wa pili aka gomea kushiriki kwa sababu ya dosari na makosa mengi ya uchaguzi wa kwanza yalikuwa hayaja tatuliwa.
SWALI:-
Sasa hapa anataka kuji apisha kama rais kwa ushindi wa kura zipi(Uchaguzi wa kwanza au wa pili)
 
Patanuka lakini na watu kuuawa tena, huyu jamaa yenu sijui vipi anakosa busara kiasi hiki
Kama vile Raila karukwa na akili.Mie nawaza:Akishaapishwa atakwenda ikulu ipi?Halafu eti anaapishwa kwa sababu kuna wakenya waliuwawa siku alipowasili Kenya kutoka ng'ambo.Natarajia kati ya leo 8/12/2017 mpaka 11/12/2017 Raila na kikundi chake watapata akili na kuachana na huo mpango kitoto wa eti kuapishwa kuwa rais.
 
Vyuma vimekaza kweli. 1academ hii picha yako ya utabiri nahisi ndo ilomfanya Raila ahairishe siku ya kujiapisha kwake. Wele wele! 😉
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…