Mwanasheria Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar - serikali tatu okay, serikali mbili ni ghali

Mwanasheria Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar - serikali tatu okay, serikali mbili ni ghali

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
othman-masoud-othman.jpg

Mwanasheria mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othman Masoud ameponda mfumo wa serikali mbili kuwa ni ghali na inawagharimu zaidi Wazanzibar kuliko wa bara ikiwepo usumbufu wa kushinda wanafuatilia masuala muhimu bara.

Kitendo cha serikali ya Tanganyika kujificha ndani ya serikali ya Muungano si uwazi.

Kwa habari zaidi soma Habari Leo Jumapili
 
[h=1]Serikali tatu pekee ndiyo itatupa amani[/h]
Dodoma.
Watanzania wameaswa kuwa makini na kuukubali mfumo wa Serikali tatu kwani ndiyo pekee utakaoondoa malalamiko na kero za Muungano.

Mbali na hilo wametakiwa kukumbuka na kuzionea huruma fedha za walipa kodi ambazo zimetumika kulipa tume 45 na vikao 50 vilivyoketi kujadili kero za Muungano kwa kipindi chote cha miaka 49 lakini hakuna mafanikio hadi sasa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mjumbe wa Baraza la Katiba Ally Salehe wakati akitoa ufafanuzi kwa wajumbe kuhusu masuala ya Muungano ndani ya Katiba Mpya kwa wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Dodoma Mjini.

Mtazamo kuwa Serikali tatu ni kuongeza gharama si za kweli na badala yake ndiyo pekee sululisho la kuondoa kero zaidi ya 47 za Muungano ambazo zimedumu kwa muda mrefu.

Tatizo la Muungano lilianzia mwanzo muda mfupi baada ya nchi hizo mbili kuungana licha ya kuwa hakuna Watanzania ambao wamewahi kuulizwa mustabali mzima wa Muungano ndiyo maana tume iliona ni vema kuliweka katika Katiba Mpya.

Mfumo wa Muungano huo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 49 bado una mambo ambayo yamefichika na kutolea mifano ya baadhi ya Mawaziri kuwa licha ya kuchapa kazi lakini upande wa pili wanaonekana kuwa hawafanyi kitu.

"Hebu fikiria hata Magufuli (Waziri wa Ujenzi) amejenga barabara ngapi Zanzibar, je huyu wa Wizara ya Afya amejenga Zahanati ngapi kule Zanzibar, lakini hawa wote wanaitwa ni Mawaziri na wanaingia katika Bunge la Muungano sasa hapa kama si kimvuli ni nini," alihoji na kuongeza:..

Aliwakumbusha Watanzania kuwa inashangaza kuona Makamu wa Rais na Waziri wa kushuhulikia Muungano lakini hana mamlaka ya kuingia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 
Serikal Tatu haitoondoa kero za Muungano bali itapunguza tu so Vikao na tume vitaendelea kama kawaida kama tunataka kukomesha kabsa Ufisad wa Vikao na Tume hizi basi hatuna budi kuhitimisha Muungano kisha tukutane kwenye Jumuia ya East Africa ambayo haina tume za aina hiyo, huyo AG asihoji barabara za Maguful pekee ahoji ni Wa znz wangapi wanamiliki Ardhi bara wakat wa Tanganyika hawana ruhusa walau ya kukod Kipande cha Ardhi znz, Watanganyika hawaruhusiwi kupiga kura kuchagua uongoz wa znz hata kama unaishi huko lakin huku wa znz wana haki zote za kuchaguliwa Tanganyika, Znz ina wawakilish special kutoka znz kwny bunge la muungano bara hawana, mbaya kuliko zote Anaependelewa ndo ana paza sauti kila kukicha eti anaonewa, dawa ya Kero ni Talaka tatu tukutane EA, AU na UN!
 
Songoro ukisikia kivuli chenyewe ndo hicho mznz bar apiga kura bara ila serekali ya znz haiwez KUPOKEA,KUOMBA MSAADA BILA TANGANYIKA KUTOA RUHUSA,JE UMEMKUTA WAZIRI ZNZ AKITIA SAINI MKATABA WA KUMATAIFA,naandik msg hii binafsi namiliki nyumba Mozambiq je TUMEUNGANA JENGA HOJA SONGORO waznz tuko tayar muungano uvunjike dogo hilo kwetu na tutamshkuru ALLAH KW NEEMA HIYOO
 
Huyu binamu yake na sefu huyu anamakando kando yake mengi kweli yeye mawazo yake yote kuwa mwanasheria mkuu wa zanzibar make kelele zote hizo ni kutaka avunje muungano ili awe mwanasheria mkuu wa kwanza wa zanzibar,

yeye anaangalia maslahi yake tu bila maslahi ya wazanzibar kazi tunayo na hawa wasomi wetu.
 
Watanzania wengi kila wanachofanya wanafanya kwa kulenga maslahi ambayo yeye anayaona ni ya mhimu kwake wala siyo kwa taifa zima.
 
Ni bora tubaki ktk mfumo wa serikaki mbili lkn cha msingi kuwe na muungano wa mkataba km vitu saba ndio tushirikiane navyo ni
Uraia
Ulinzi
Currency
Forodha
Nk
Hili linaweza kuwa ndio jambo litakaloondoa kero za muungano kwani kuja na serikali tatu zanbar itadai maslahi yake km eneo lake la zenji empire kuanzia mwambao wa afrika mashariki ikiwemo dar kilwa,mombasa ,bwagamoyo .tanga .hadi msumbiji ,kiti chake umoja wa mataifa ndo hiki cha tanzania,tanganyika hawana kiti umoja wa mataifa hapo ndipo kitapoeleweka na mafujo yatakapo anza
Muungano wa mkataba ndio suluhisho la kero
 
mi naona bora tuwe na serikali mbili yaani Tanganyika na Zanzibar na kila moja iwe na mamlaka kamili, yes muungano uendelee kuwepo ila muungamo wa mambo machache kama tulivyo katika East Africa community
 
Songoro ukisikia kivuli chenyewe ndo hicho mznz bar apiga kura bara ila serekali ya znz haiwez KUPOKEA,KUOMBA MSAADA BILA TANGANYIKA KUTOA RUHUSA,JE UMEMKUTA WAZIRI ZNZ AKITIA SAINI MKATABA WA KUMATAIFA,naandik msg hii binafsi namiliki nyumba Mozambiq je TUMEUNGANA JENGA HOJA SONGORO waznz tuko tayar muungano uvunjike dogo hilo kwetu na tutamshkuru ALLAH KW NEEMA HIYOO

Kwahiyo unakubaliana na Songoro kwamba njia pekee ya kutatua matatizo ya Muungano, ni kuuvunja huu Muungano wa ki-nafique?
 
Back
Top Bottom