Mwanasheria Mkuu Tanzania agaragazwa kesi ya ubunge EAC

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925


JOPO la Majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki, limemwamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania kujibu hoja zilizowasilishwa mahakamani hapo na Anthony Komu (CHADEMA) ndani ya siku 15 na kumlipa mlalamikaji huyo gharama katika hatua za pingamizi za awali. Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji watatu, Johnston Busingye, Marystella Amoko na Jean Bosco Butasi katika mahakama hiyo jijini Arusha ambapo upande wa serikali uliwakilishwa na wakili Mark Mwalambo na upande wa mlalamikaji unawakilishwa na wakili Edson Mbogoro.


Katika kesi hiyo ya marejeo namba 7 ya mwaka 2012 iliyofunguliwa katika mahakama hiyo, Komu ambaye alikuwa mgombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, anapinga utaratibu uliotumika kupata wagombea wa ubunge kutoka Tanzania kwani ulikiuka ibara ya 50 ya Katiba ya Afrika Mashariki inayosema kuwa wabunge watapatikana kwa uwiano. Awali Januari 31 mwaka huu katika mahakama hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alilalamikiwa mahakamani hapo kwa kushindwa kujibu hoja ndani ya siku 45 alizopewa.


Katika utetezi wake, Mwanasheria Mkuu alitoa sababu nne za kwa nini hakujibu ndani ya muda aliopangiwa, akisema kuwa kulikuwa na kesi kama hiyo ikisikilizwa mjini Dodoma, na kwamba alitoa sababu kuwa walikuwa hawajajua viwango vya ada za kesi hiyo. Aliongeza kuwa walikuwa wanatafuta wanasheria wa mahakama ya Afrika Mashariki ili waweze kupata tafsiri za kisheria kwa mambo yaliyowasilishwa. Katika sababu ya mwisho alidai kwamba kwa kuwa suala hilo lina maslahi ya nchi na jumuia yenyewe, ilibidi liangaliwe kwa umakini ili Tanzania isikose haki.


Madai hayo yote yametupiliwa mbali na jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo, hivyo kumuamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujibu hoja zilizotolewa mahakamani hapo ndani ya siku 15 na kulipa gharama za mlalamikaji.



 
Dah aibu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kichwa siyo kwa ajili ya kufugia nywele tu jamani pia hutumika kufikiria
 
Ngoja atiwe adabu amezoea kuwaburuza watanzania pale Bungeni
 
Kilaza wa Tundu Lissu ni Werema daima!! Nchi inapata aibu jamani kha!!! Cant afford the quality?!
 
Hata ile kesi ya mpaka na Malawi akisimamia huyu mccm tumeumia . Hamna kitu hapa
 
Haya sasa, mimi nilimuona bungeni anamapungufu sana!
 
ukiwa kama baba umepoteza imani kwa watoto wako,na ushukuru sipo nao jirani wangejuta kwa takataka zako
 
Haya maji anayoonekana akiyanywa ni kwasababu maji hayana utashi bila shaka kama yangekuwa na akili yangeshafahamu kwamba hayastahili kuingia kwenye tumbo la kilaza mtia hasara hata hewa anayovuta hapa duniani haina manufaa kwa mtu yeye zaidi kuimarisha uwepo wa nyang'au hili....Linachukiwa Nchi Nzima lakini halijitambui pumbaaaaaavu zake
 
Ratizo sio kichwa ni nywele
Nilishawahi kuandika hapa jamvini kuwa huyu jamaa ni kilaza wa mwisho. Pia amethibitisha ile kauli yake mwenyewe kuwa kazi ya kichwa sio kufugia nywele tu, kumbe jamaa huwa hatumii kichwa kufikiri bali kufugia nywele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…