Mwanasheria Mkuu wa Marekani ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Marekani ajiuzulu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr, mmoja wa washirika wakubwa wa Rais Donald Trump, anajiuzulu wakati kukiwa na mvutano wa muda mrefu na rais juu ya madai yasio na msingi ya rais ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uliomalizika na uchunguzi juu ya mtoto wa rais mteule Joe Biden.

Barr alikwenda siku ya Jumatatu White House, ambapo Trump alisema mwanasheria mkuu huyo aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Trump ameonyesha hasira yake hadharani juu ya taarifa ya Barr aliyoitoa kwa shirika la habari la Associated Press mapema mwezi huu kwamba Idara ya Sheria haikuona udanganyifu mkubwa wa uchaguzi ambao ungebadilisha matokeo ya uchaguzi huo.

Trump anasema Naibu Mwanasheria Mkuu Jeff Rosen atakuwa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Trump bado hajakubali matokeo bado, anapanga mapinduzi baridi, anaogopa hatima yake baada ya Urais, amebakisha karata moja kucheza kupitia makamu wake wa Rais katika Senate abadilishe matokeo ya kura ili aendelee kutawala.

Barr amejiondoa kwa kuogopa aibu ya kushindwa na kushitakiwa, Mwanzo wa Mwisho wa enzi za Trump.
 
🤣🤣🤣
7654321.jpg
 
Trump bado hajakubali matokeo bado, anapanga mapinduzi baridi, anaogopa hatima yake baada ya Urais, amebakisha karata moja kucheza kupitia makamu wake wa Rais katika Senate abadilishe matokeo ya kura ili aendelee kutawala....
Hiyo sio Africa, hakuna mashitaka yoyote hapo,hao tayari Wana strong institutions hivyo Rais kufanya nje ya mfumo very rarely
 
Alibakiza mwezi mmoja so sio kujiuzulu amestafu kwa kutaka mwenyewe.
 
Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr, mmoja wa washirika wakubwa wa Rais Donald Trump, anajiuzulu wakati kukiwa na mvutano wa muda mrefu na rais juu ya madai yasio na msingi ya rais ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uliomalizika na uchunguzi juu ya mtoto wa rais mteule Joe Biden.

Barr alikwenda siku ya Jumatatu White House, ambapo Trump alisema mwanasheria mkuu huyo aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Trump ameonyesha hasira yake hadharani juu ya taarifa ya Barr aliyoitoa kwa shirika la habari la Associated Press mapema mwezi huu kwamba Idara ya Sheria haikuona udanganyifu mkubwa wa uchaguzi ambao ungebadilisha matokeo ya uchaguzi huo.

Trump anasema Naibu Mwanasheria Mkuu Jeff Rosen atakuwa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr, mmoja wa washirika wakubwa wa Rais Donald Trump, anajiuzulu wakati kukiwa na mvutano wa muda mrefu na rais juu ya madai yasio na msingi ya rais ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uliomalizika na uchunguzi juu ya mtoto wa rais mteule Joe Biden.

Barr alikwenda siku ya Jumatatu White House, ambapo Trump alisema mwanasheria mkuu huyo aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Trump ameonyesha hasira yake hadharani juu ya taarifa ya Barr aliyoitoa kwa shirika la habari la Associated Press mapema mwezi huu kwamba Idara ya Sheria haikuona udanganyifu mkubwa wa uchaguzi ambao ungebadilisha matokeo ya uchaguzi huo.

Trump anasema Naibu Mwanasheria Mkuu Jeff Rosen atakuwa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Uzee site ghazab ila dhahabu
 
Watu wa aina hii hapa kwetu hawajazaliwa! The Beutiful Ones Are Not Yet Born
 
Hawataweza, anazani kule ni Afrika, Trump anachofanya ni kuendelea kuchangisha pesa ili zije kumsaidia 2024 hana jipya hata yeye anaamini hakushinda sema tu, wanachama wengi wa Republican ni wanaelimu ya chini ni rahisi kudanganywa

Back
Top Bottom