Mwanasheria mkuu wa Serikali ameapa kiapo cha uaminifu Bungeni

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameapa kiapo cha uaminifu bungeni leo Agosti 27, 2024.

Ameapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge.

Hamza aliteuliwa na Rais, Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Agosti 14, 2024 akichukua nafasi ya Jaji Eliezer Feleshi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Soma Pia: Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

Kabla ya uteuzi huo, Johari alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

Mwanasheria Mkuu ndiye mshauri mkuu wa kisheria wa Serikali na Bunge akiwa na jukumu la kusimamia masuala ya kisheria.
 
only in Tanzania mwanasheria mkuu ambaye hajawahi kukanyaga mahakamani wala hayuko kwenye practice tangu aajiriwe sirikalini kisa babaake Johari, basi sawa.
 
Back
Top Bottom