Mwanasheria Mkuu, Mhe Werema anayo haki ya kufurahisha nafsi yake lakini si kuamua juu ya hatima ya KATIBA ya nchi.
Huyu bwana anayo wajibu tu wa kuishauri serikali juu ya KATIBA ikishapatikana. Lakini pale KATIBA inapotafutwa, yeye kutoa juu ya HATIMA ya andiko hili ni to act ULTRAVIROUSLY bila ya ulazima. Hatujamsikia akizungumzia Mbunge anapopigwa na polisi, kwa nini adandie kazi si yake hapa??
Katiba si mali ya Werema, Katiba si Mali ya Kikwete na Mwinyi wala Katiba si mali ya Serikali.
Kama walivyowahi kusema Waheshimiwa Prof Lipumba, Dr Slaa, Duni Haji Duni, Wasomi kibao na Wanasheria waliotukuka, KATIBA ni mali ya Mtanzania wa kawaida. Lini akalirekebishe na kwa mtindo gani yote ni juu yake mwenyewe kuamua.
Mwanasheria Mkuu ni mwajiriwa wa KATIBA na hana msingi wa kumamulia mwajiri wake kitu gani akafanye juu ya KATIBA. Wapinga MABADILIKO YA KWELI nchini, hebu tukutane bungeni Dodoma.