Mwanasheria Mkuu Zanzibar atupilia mbali hoja ya Sendeka

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482

Mwanasheria wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Othuman Masoud, ametupilia mbali hoja ya mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Christopher Ole Sendeka, la kutaka hati ya Muungano kutoonyeshwa hadharani, badala yake iwe siri.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Sendeka kupinga hoja ya John Mnyika ambaye alitaka kanuni ziweke wazi upatikanaji wa nyaraka mbalimbali za kitaifa ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa hati ya maridhiano ya Muungano.

Baada ya Mnyika kutoa hoja hiyo, Sendeka alipinga pendekezo hilo kutaka ufafanuzi wa kisheria kutoka kwa Kamati ya Kumshauri Mwenyekiti wa Muda kuhusu kanuni za Bunge hilo kama kweli ni sahihi hati ya Muungano kuwekwa wazi.

Masoud alisema hakuna tatizo lolote la upatikanaji wa hati ya Muungano kwani hati hiyo ni wazi kwa Watanzania wote.

"Labda kama mjumbe (Sendeka) anazungumzia hati nyingine ambayo si ya Muungano wa Tanzania, lakini kama ni Muungano huu ambao mimi naujua, sioni kama kuna tatizo lolote ambalo linazuia kupatikana kwa hati hiyo na kuisoma kwa hati hiyo ni taarifa ya wazi kwa Watanzania wote," alisema.





CHANZO: NIPASHE
 
Zile zama za USIRI USIRI zinaanza kwisha. Bado mikataba kati yetu na wawekezaji.
 
Hawa CCM naona wanajichanganya sasa, yani wanataka vitu vya wazi viwe SIRI na vya siri viwe WAZI. Hati ya muungano siyo siri, na ndiyo itasaidia kurekebisha kero zilizopo kwenye muungano. Swala la kura ni siri, ila hawa CCM wanataka liwe wazi. Hivi kumbe huu muungano ulikuwa ni wa SIRI.
 
Sendeka anastahili laana. Michango yake bungeni mingi ina maslahi binafsi na si kwa maslahi ya watanzania wa kawaida.
 
Huyu Sendeka atatuingiza kwenye matatizo makubwa kwa mwendo wake tunaweza tusipate katiba kwa wakati maana naona anajidanganya kila kitu anakijua na kama yeye ndo msemaji sana wa kila kitu. Amejaa mawazo ya zamani yasiyoangalia hatma ya nchi hii miaka 50 ijayo.
 
Tatizo la Sendeka ni tumbo kuongoza kichwa
 
Ole Sendekea mwisho wa Ubunge wake ni September 2015
 
Hili Bunge lingeendelea kuongozwa na mzee Kificho wabunge wengi wa CCM wangeumbuka kwa sababu wamezoea kuvunja taratibu na kanuni za bunge wanaachwa na akina Makinda na Werema! Siku hizi wanapewa za uso wakichangia pumba!
 
Hili Bunge lingeendelea kuongozwa na mzee Kificho wabunge wengi wa CCM wangeumbuka kwa sababu wamezoea kuvunja taratibu na kanuni za bunge wanaachwa na akina Makinda na Werema! Siku hizi wanapewa za uso wakichangia pumba![/QUOTE


Mkuu umenena vema.
 
Hili Bunge lingeendelea kuongozwa na mzee Kificho wabunge wengi wa CCM wangeumbuka kwa sababu wamezoea kuvunja taratibu na kanuni za bunge wanaachwa na akina Makinda na Werema! Siku hizi wanapewa za uso wakichangia pumba!

Nitamkumbuka sana mzee Kificho kwa hekima na busara zake ktk kuongoza watu mchanganyiko
 
tatizo la sendeka ni miongoni mwa mazuzu wanaojua hii nchi ni ya ccm wengine ni wapangaji tu,na zaidi ni jitu la kupenda sifa za kijinga mbaya zaidi joga mno.
 
Ukishakuwa kiongozi kupitia CCM suala la kupindisha seria au kanuni kwa manufaa ya CCM wala sio suala la kushangaza.....ni jadi na ndio fahari yao,sasa anapotokea mtu kama Kificho mwenye misimamo ya Ki-Nchi basi wanamuona kero kweli.....na angekuwa wa kudumu lazima angeundiwa zengwe.....
 
Ccm wanahaa.pole pole mungu anawaadhibu .siri gani ulifichwa miakanendarundi sasa mda umefika uwekwe wazi
 
Kakke,

..kwa kweli ktk bunge hili wabunge toka ZNZ,haswa wale wa CUF, wananifurahisha sana.
 
Last edited by a moderator:

Teacher;
Naona weye ni Mwl. kweli kweli. Unalijua jambo kabla halijawa. Huyu Bwana, Mhishimiwa sana Ole Sendeka, anayo matatizo ya Kimila na desturi za kikwao. Anapopokelewa kama mungu kwao anadhani kila mahali ndivyo wanatakiwa wamwone. Yaani mmasai mpaka Bungeni.
CCM ndivyo wanavyo mwona kwani kila anapompinga mbunge mwingine kutoka upinzani wakampigia makofi anajiona kuwa anasema kwa hekima kuubwa kumbe ni pumba tu.
Kura ambayo ndiyo ingetakiwa iwe siri ili kuufungua moyo wa huyo mpiga kura, kama tunavyofanya hata tulipomchagua yeye kuwa mbunge kwa siri hiyo ameipinga anataka iwe ya wazi ili hao mabwana zake walio mchagua aingie hili bunge la katiba wamwone akiwa saport kwa kila ujinga wao. Lakini, Hoja ya maridhiano hayo ya huo Muungano kuwekwa wazi kwake ni vibaya, kwani anatuona kuwa hatujui hata kusoma na kuandika ila yeye tu ndo maana yupo huko bungeni.
Tunampa Pole zake, asubiri vijana wamuumbue kwa hoja maridhawa.
 
Hili hili liSendeka linaongea hadi koo linataka kukauka liking'ang'ania upigaji wa kura uwe wazi, Leo kwenye suala muhimu kama mkataba wa muungano linataka iwe siri, CCM ni janga..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…