Uchaguzi 2020 Mwanasheria wa ACT Wazalendo: Msajili hawezi kukifuta chama

Uchaguzi 2020 Mwanasheria wa ACT Wazalendo: Msajili hawezi kukifuta chama

saidi kindole

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2012
Posts
310
Reaction score
792
Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo, Omar Said Shaaban ametolea ufafanuzi juu ya Msajili wa Vyama kufuta usajili wa chama.Kupitia akaunti yake ya Twitter amesema haya.

Ufafanuzi: "Kifungu cha 19(3) cha sheria ya Vyama vya Siasa inasema mamlaka ya msajili kufuta usajili wa chama cha siasa hayawezi kutekelezwa ikiwa kipindi kilichobaki kuelekea uchaguzi hakizidi miezi 12."

Shabani.JPG
 
saidi kindole,
Hivi ni kweli hicho Kifungu cha Sheria walisahau kukifuta au kukirekebisha kwa kipindi cha hii miaka mitano? Hata siamini! Du!
 
Ccm mtasema mmefumbwa macho hamuoni matendo yenu ya unyanyasishaji. Wananchi wanahasira sana wananung'unika moyoni. Kamwe huwezi kuongoza nchi kwa mkono wa chuma ukawa salama
 
Mwisho wa ccm unakuja na unaletwa na wao wenyewe na hawataamini.
 
Tutarajie wanachama wengi zaidi wakikatwa kwenye kura za maoni!
 
Kama tunafuta vyama kwa hiyo tujipange kupita bila kupingwa...
 
Uchungu wake ni kumuona mwenye ndevu ametangaza kugombea tena urais, hili linamnyima usingizi sana nadhan mkataba wake walifikia makubaliano afanye vyovyote iwavyo jamaa asigombee baada ya kumnyanganya chama hakutegemea kilichotokea kwamba siasa ina upande wa pili wa shilingi.
 
Anaweza kufuta makusudi kisha waende mahakamani. Wasumbuliwe weeeeeeee na mapingamizi weeeeeee mpaka mwakani then haki inapatikana ACT Wanashangilia
 
Uchungu wake ni kumuona mwenye ndevu ametangaza kugombea tena urais, hili linamnyima usingizi sana nadhan mkataba wake walifikia makubaliano afanye vyovyote iwavyo jamaa asigombee baada ya kumnyanganya chama hakutegemea kilichotokea kwamba siasa ina upande wa pili wa shilingi.
Kwani Jecha aliondoka na ule ufutio?
 
Jamaa aliwachenga kwa mwili hawakutegemea
Uchungu wake ni kumuona mwenye ndevu ametangaza kugombea tena urais, hili linamnyima usingizi sana nadhan mkataba wake walifikia makubaliano afanye vyovyote iwavyo jamaa asigombee baada ya kumnyanganya chama hakutegemea kilichotokea kwamba siasa ina upande wa pili wa shilingi.
 
Please mwenye link yenye barua anitag please. Nimeitafuta mpaka nimechoka
 
Back
Top Bottom