Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick, ametoa ufafanuzi juu ya umiliki wa mchezaji Yusuf Kagoma baada ya mazungumzo marefu na klabu ya Singida Fountain Gate. Patrick alisema, "Tulianzisha maongezi ya muda mrefu na Singida Fountain Gate kwa lengo la kununua rasmi Yusuf Kagoma."
Kwa mujibu wa Patrick, Singida ilitoa masharti ya kulipa shilingi milioni 30, na Yanga ilikubaliana kufanya malipo hayo kwa awamu mbili. Malipo ya kwanza yalifanyika tarehe 30 Aprili, na baada ya hapo, klabu ya Yanga ilipewa ruhusa ya kuzungumza na mchezaji kuhusu maslahi yake binafsi.
Baada ya makubaliano hayo, Yanga ilimtumia Kagoma tiketi ya ndege ili afike Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini mkataba. Kagoma alifuatana na wakili wake, Bwana Léonard, na akaweka saini yake rasmi.
Kwa mujibu wa Patrick, "Tunaweza kusema Kagoma bado ni mchezaji wetu."
Chanzo: Crown FM
Soma pia;
=> Sakata la Yusuph Kagoma kusaini timu mbili Klabu ya Simba kukatwa alama
=> Mwigulu awaomba viongozi wa Yanga wapotezee suala la Kagoma ili aweze kucheza Simba
=> Ahmed Ally atoa kauli kuhusu sakata la Yusuph Kagoma na Yanga SC