Mwanasiasa Caren Atieno Muga akamatwa akiwa kwenye harakati za kukimbia kwa kesi ya kuvuna na kuuza viungo vya binadamu

Mwanasiasa Caren Atieno Muga akamatwa akiwa kwenye harakati za kukimbia kwa kesi ya kuvuna na kuuza viungo vya binadamu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Kenya nini kinaendelea huko majirani?

Caren Atieno Muga, aliyekuwa MCA mteule wa Kaunti ya Kisumu, amekamatwa baada ya kuhusishwa na sakata ya uvunaji na uuzaji wa viungo vya binadamu.

Bi. Muga alikamatwa akiwa barabarani katika eneo la Chemelil-Miwani-Kisumu wakati akijaribu kutoroka nyumbani kwake, baada ya kupashwa habari kuhusu uvamizi wa polisi uliokuwa ukipangwa kufanyika katika makazi yake.

Kulingana na taarifa za polisi, mwanawe Bi. Muga ni mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji ya hivi karibuni, mauaji ambayo Enock Kipsang, aliuawa kikatili kwa kukatwa kichwa na sehemu za siri eneo la Chemase, Kaunti ya Nandi.

buzz.png

Mmoja wa washukiwa wa mauaji hayo, Victor Kimtai, alikamatwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Chemase. Hata hivyo, alitolewa kwa nguvu kutoka selo na umati wa wananchi wenye hasira waliovamia kituo cha polisi na kuwazidi nguvu maafisa wa polisi, kisha wakamchoma hadi kufa.


Gari alilotumia Bi. Atieno kutoroka, aina ya Toyota Harrier, limepelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kapsabet kama ushahidi wa tukio hilo.

Source: Buzzroom Kenya, Citizen DIgital
 
Wanasiasa wa kiafrica hao
Kesi zao huwa zinaendelea miaka haziishi hawa. Fuatilia kesi zao kuanzia yule gavana aliyemuua binti wa chuo aliyekuwa na mimba yake, mke wa marehemu cohen yule bilionea mzungu aliyeuawa na mkewe kisha kuitupa maiti kwenye ceptic tank ili achukue mali, kesi ni nyingi sana huwa hazihukumiwi na hii bila shaka haitaisha atarudi uraiani.
 
Kama ni kweli anajishughulisha na huo ushetani, basi na sheria nayo ichukue mkondo wake.
 
Back
Top Bottom