TANZIA Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Njelu Kasaka amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Mbeya alipokuwa akipatiwa matibabu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Masache Kasaka amethibitisha kifo cha Baba Yake kwa kusema amefariki dunia kutokana na tatizo la moyo lililokuwa linamsumbua. “Wakati anaedelea na matibabu katika hospitali akapata mshituko wa moyo uliosababisha kufariki dunia,” . Msiba uko nyumbani kwake, Chunya mkoani Mbeya, “na mazishi yatakuwa Jumapili (tarehe 5 Julai,2020).”

Kasaka ambaye amepata kuwa mbunge, Waziri na mkuu wa mkoa, alijitoa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015 na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kugombea ubunge jimbo la Lupa.

Mwaka 2019, Kasaka alizindua kitabu chake alichokiita ‘Njelu Kasaka: Maisha, Siasa na Hoja ya Tanganyika-G55.”

Mzee Njelu Kasaka ameacha watoto saba na mjane mmoja.

Baada ya kusoma makala yake nikaisaka CV ya Njelu Kasaka

Njelu Kasaka: Hakuna aliye salama ndani na nje ya CCM

Njelu Kasaka ajiunga na CHADEMA

Wako wapi G55?

 
Umri? Next time ulizia umri wa marehemu kwanza kabla ya kukimbilia kuhabarisha.

Apumzike kwa Amani!
 
Nadhani aliwahi kuwa mbunge wa Chunya na pia aliwahi kuwa waziri wa kilimo na ushirika kwenye serikali ya Mwinyi.
Mmmm huyu atakuwa mkongwe sana sijawahi msikia hata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…