Mwanasoka gani wa bongo unahisi alistahili au anastahili kucheza Ulaya?

Probably niko off target kidogo, Huwa namfuatilia samatta anavocheza kwenye team yake ya sasa hivi (KRC Genk) halafu naangalia baadhi ya stikers pale EPL ambao kwa mtazamo wangu hawamfikii hata robo.. kwa mfano berahino wa stoke city.
Samatta ni pure talent aendelee ku-step up we need to see him kwenye bigger stages akiperform.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Zaidi hata ya Zamoyoni Mogella??
Hawa mafundi wawili c wakulinganishwa kwasababu kila mmoja anacheza nafasi tofauti na mwenzake, isitoshe kila mmoja alikuwa fundi katka nafasi yake.Ni sawa na kuwalingalinsha Zamoyoni Mogela, Edibilly Jonas Lunyamila na Juma Pondamali Mensah.
 
Alisoma Shycom Shinyanga
 
Haruna Moshi Boban
Kelvin Yondan
Athuman Idd Chuji
Victor Costa
Selemani Matola
Ibrahimu Ajibu
Zamoyoni Mogela
Said Mwamba Kizota
Peter Tino
Boniface Pawassa
Wengi Sana...
Umechemsha sana sababu hawakuwa na sifa za kucheza nje Mogela aliishia Arabuni tu na Kizota arabuni kwenye ligi za Mafuta tu
 
Hahaha hapa nachoona ni vita ya simba na yanga kutukuza ma-legendary wao...
 
Method Mogela na Hamis Gaga ( kama angekuwa na discipline ya mchezo)
 
Kama Nonda shaban alicheza ulaya, basi Edibily Lunyamila alistahili pia kucheza ulaya.
 
Kuna aliyewahi kumsikia au kumfahamu Jumanne Masimenti?
Huyo jamaa alikuwa ni shida unaambiwa. Hafanyi mazoezi, na ni mhuni au tumwite msela,ila tabia chafu tu kwa ujumla.
Na ilipelekea kutopendwa na makocha na hata timu ya Taifa hakuwahi kuitwa! Ila mweke uwanjani uone shughuli yake
 
Ila wako wengi, na naamini Said Mwamba "Kizota" asingekosa timu Ulaya
 
Hawa wa sasa sioni mchezaji mkali kabisa kiviiile.. Maana hawafikii kiwango cha waliocheza zamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…