Mwanaume aliyelelewa na mama peke yake, ni mtu wa aina gani?


Nimesha msamehe buree ndo mana sitaki hata kumuona..kwanza nimsamehe ili iweje??
 
well said Yummy! pokea ma-like kama 10 hivi! niliona hapa mtu akisema hawezi oa mtu aliyelelewa mama peke yake, and i was like whaaaaatttt?? kwa kweli ni unyanyapaaji wa hali ya juu, tuwaache watoto, hawahusiki kwenye ufirauni wetu.
 
Last edited by a moderator:
Baba atabaki kuwa baba tu ata kama alukutenda nini kuna waliofanyiwa ukatili mkubwa na baba zao na wakasamehe sembuse wewe sio kosa lako,inua mdomo wako umtukane unavyoweza umlaani unavyoweza hatapata madhara lakini siku atakapo inua mdomo wake na kukulaani iyo laana itakutafuna mpaka unaingia kaburini haijalishi alikutunza au hajakutunza,ni hayo tu.
 
Hata wanaolelewa na wazazi wote wako kama hawa pia...........tena wamelelewa kwenye maisha mazuri tu wala sio kwamba shida ndio zimempelekea kufanya hivi. Narudia tena tumshirikishe Mungu kwenye malezi ya watoto wetu hamna wa kujisifia hapa mimi najua kulea vizuri zaidi ya wewe.......
 

@gfsonwin ahsante kwa maelezo yako mazuri..........
Binafsi ninamuangalia mama Ben Carson kama mama Shujaa.

kwa nini?

*Aliolewa akiwa na umri wa miaka 13 na mchungaji mzee kwa kukimbia shida za pale nyumbani kwao, ambapo pia aliachika na kuachiwa kuwalea watoto wawili pake yake.

*Mama huyu aliishia darasa la tatu, ambapo sio kiwango kizuri cha elimu cha kujivunia, lakini kwa shida sana alilazimika kufanya kazi zaidi ya tatu ili ahakikshe anawatengenezea wanae hao future.

*Carson alikuwa mbumbumbu darasani, lakini kutokana namsimamo wa mama yake wa kuwalazimisha kusoma libarary, alipata mwamko na kusoma kwa bidii hadi kufikia kuwa daktari bingwa wa upasuaji.

Haya ni mafanikio makubwa kwa mama huyu (Mwanamke huyu) ambaye hakupata elimu kubwa. Je kuna wazazi wangapi ambao wana elimu ya kutosha tu lakini malezi kwa watoto wao yamewashinda?

Hata hivyo naomba nikiri kwamba, wapo kina mama wengi sana ambao kwa juhudi kubwa wamefanikiwa kuwalea watoto wao wakiwa peke yao, baada ya kutelekezwa na wenzi wao au wenzi wao kutangulia mbele ya haki na watoto hao wamekuwa ni mfano bora wa kuigwa.

Naomba wote tuwapongeze kina mama hawa na kuwapa sifa zinazostahili..........
 
Mmmh, huyo mtoto wa kiume anayetakiwa kukopi tabia za baba, kwani mababa wote wana tabia za maana sasa za kukopi?
Hadi imefanye wanamme aliyelelewa na mama kuwa 'less'?
 
Hivi unaweza anza kujenga paa kabla ya msingi?

Haitakuwa nyumba tena bali kibanda cha mabati hata hivyo kinaweza kukinga na jua au mvua japo si nyumba.

mkuu kuna wakati unajihisi kama una mapungufu fulani kwa kitendo cha baba kuwa mbali na wewe utotoni? na vipi baba akija sasa hivi na kutaka kujenga uhusiano na wewe,utamkubalia?
 
Hapa ndio naaami kwamba umelelewa na mama na alichokosea mama yako ni kukufundisha tabia za kike majibu yako ni kikekike tu bila shaka utakuwa umefanana na hizi picha za hawa jamaa hapo juu.
 
Mbona kuna ndoa ambazo wazazo wapo wote lakini mama ndiye anayewajibika zaidi. wakati baba hajui hata mtoto yuko darasa la ngapi! wala anavaa na kula nini! MAMA NI MAMA NA HAKUNA MFANOE!
 
Pole sana kwa yaliyokukuta ndugu, but matatizo ni mengi sana duniani, hutakuwa wa kwanza wala wa mwisho kutokewa na matatizo cha msingi mshukuru Mwenyezi Mungu kukufikisha hapo japo hukupata mapenzi ya pande zote, usikufuru na kumtolea lugha chafu mzee wako (maniner zake) samehe kama una dini, na mwache babako na Mungu wake, kila jambo litokealo duniani lina sababu zake, may be angekulea usingefika hapo ulipofikia, so think twice............

  • :thinking:
 
Ninachokiona kwenye thread hii watu wameamuwa kubwabwaja na kumalizia misongo yao ya maisha hapa. Ukweli halisi wa mtoto kulelewa na mama ni huu:

Kuna mazingira mengine ambayo yanasababisha watu msiishi pamoja na mkiwa tayari mna mtoto, lakini mwanaume una clear bill zote zinazomuhusu mtoto kuanzia school fees, mavazi na daily nourishment.

Kuna baadhi ya cases kina Mama hawana guts za kuwaeleza ukweli watoto/mtoto wao ni kwa nini hawaishi pamoja na Baba yake na kumueleza kiunaga ubaga kwamba Baba yako ndiye anayeclear bill zote za kukulea, hapa kwa mwanamke mwenye akili unakuwa unayajenga mapenzi ya mtoto kwa Baba yake hata kama atakuwa anakutana naye mara moja kwa moja.

Through my experince baadhi ya wanawake hasa wenye vijiajira vya kujikimu si wakweli na hawawaelezi watoto zao ukweli, utafuta sifa za kijinga kwamba yeye ndio kila kitu kwa mtoto, hizi ni sifa za kijinga.

Kuna mtu hapa analalamika Baba yake hamjali, am sorry bro lakini kwenye ukweli uongo ujitenga, huyo si Baba yako bali Mama yako alimsakizia tu hiyo Mimba, sisi kama Wazazi hakuna important thing zaidi ya mtoto. Nimekuwa nikifuatilia kwa makini sana hasa wasanii akifanyiwa Interview watu wa kuwashukuru lazima atamtaja Mama yake lakini Baba hatotaja, na hata nikiwauliza je mnajuwa Baba yake Diamond nina uhakika hakuna hamjuwae.
 
Hii thread imenigusa sana, nina imani wanakuwa wanaume wazuri although kuna vitu vidogo wanakosa as hawajafundishwa na baba zao kwa kuona uhalisia nyumban,, my self my father passed away when I am 5 years old, so mi with my elders tumelelewa na mama alone,, tulikuwa tunapata kila kitu as we thanks God mother alikuwa na uwezo kiasi chake na mzee aliacha vitu ambavyo vilisaidia malezi,,, lakini bado tulikuwa tunamiss uwepo wa baba although shule nzuri, mavaz, magar and so on tulikuwa na access navyo,,, baba ni muhimu sana kumkuza mwanaume, and I real miss him as I wish ningekuwa nae up to this time,,, wamama wanadekeza sana hasa wakiwa na uwezo hadi mda mwingine unajishtukia kwa washkaji,
 
Matola


Green - Umetumia maneno makali sana,kama umeona amekosea ungemuelimisha lakini sio kumtamkia hivyo.....Je, wewe una uhakika na unalolisema???

Red - naomba kuanzia LEO uwe unatumia neno MIMI kama mzazi pliiiiiiiiiiiiiiz....................kuna wababa wenye watoto wao na DNA wamepima wana uhakika wala hawajasingiziwa na bado hawatoi hata sumni kuwalea hao watoto. Na utakuta wana uwezo mzuri sana wa kuwalea hao watoto,tena basi wengine hawaja jaliwa hata kupata watoto wengine.
 
Last edited by a moderator:
Nimesha msamehe buree ndo mana sitaki hata kumuona..kwanza nimsamehe ili iweje??
Mr Rocky na wengineo wote jamani tumejitahd sana kumshauri huyu mtoa mada but yaelekea moyo wake bado umefungwa na mzigo wa chuki na hasira alizoziweka taka utotoni. Najua yataka muda sana ili kusamehe so tusikwazike kwa majibu yake yenye kuonyesha hasira za wazi la tumuombee akutane na neema ya Mungu ili asamehe na kuachilia.

natangulza samahani sana kama at any point nimekukwaza kwa kauli yeyote ile.
 
sawasawa mdau, nakubaliana na wewe...huyu jamaa nimegundua ana tatizo la KUKARIRI wakati sio ishu kabisa, kwani mwisho wa siku ni akili ya mtoto mwenyewe bila kujali kalelewa na mzazi mmoja au wote...tena hao waliolelewa na mzazi mmoja huwa na uchungu sana wa kutunza familia zao ili kuepuka yaliyowatokea wao kwani wanasema uking'atwa na nyoka, jani likikugusa........so jamaa asikariri na wala haijalishi, maisha ni maisha tu hakuna aliyeomba kulelewa na mzazi mmoja au wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…