Mwanaume aliyelelewa na mama peke yake, ni mtu wa aina gani?

Mzazi wa namna hiyo anapaswa kabisa kupimwa akili zake Milembe, Baba ambaye mimi nakubali asamehewe ni hhawa wa dizaini waliopena ujauzito wakiwa shule na wote kiumri wako under 20 na isitoshe mwanaume hana kipato naye anategemea pesa za kupewa, huyu anaweza kusamehewa lakini jitu zima na akili zake na kipato chake unatelekeza mtoto!? hapa huwezi kuwa na akili timamu.

Haiingii akilini mimi nilikuwa na Girlfriend nikiwa shule lakini akaja kuolewa na mtu mwingine kwa sababu sikuwa tayari kimaisha na nilikuwa napiga deiwaka ughaibuni, lakini mpaka leo akiwa na shida ya pesa huwa namsaidia kama ninazo licha ya kwamba ana mume wake na mimi sifanyi naye kabisa ngono, ndio nithubutu kumtelekeza mtoto wangu mwenyewe?
 
Yes ni kweli huwa kuna tofauti, kimsingi huwa ni mwelewa, msikivu na huwa na huruma ambazo hurithi kwa mama ake.
 
Watoto waliolelewa na mama alone huwa ktk hatari ya kutokuwa wazazi wasiowajibika kwa watoto wao, kwani uamini mama anaweza kila kitu (kama walivyo lelewa na mama zao) hawana ujasiri hawa (huwezi kuwakuta jeshini, polisi au ktk kazi zingine za hatari) hupenda kulalamika sana hata kama makosa ni yao, huwa wanadekadeka na hawawezi kuishi na watu wengine bila mama zao, hata wakioa mama zao uendelea kuwa waamuzi ktk familia zao jambo ambalo husababisha wake zao kuwa na chuki dhidi ya mama zao,
 
the question is too philosophical,so it needs philosophical answers and not blaming!:flame:
 

Fafanua kwanza manake sasa mnaanza kunyanyapaa wliokosa bahati ya kulelewa na wazazi wawili.

Je una maana single mother kama mama ambaye hajaolewa ama hata MJANE?
 
natafuta mwanaume aliyelelewa na mama, wengi wanakuwa wapambanaji, na wanajua thamani ya mwanamke..........
 
Eeeh bhana saafi kwa hii maada but nataka kukueleza kwamba mtoto alie lelewa na mama huwa mwenye busara na mwenye uchungu na utafutaji kimaisha kwani anapozikumbuka shida alizopata na mama yake ni waz na dhaili hawez kuwa mzembe ila ktk kipengere cha kumsamehe mding huwa tunakua wagumu kutokana na kupandikizwa na mama mbegu za kutomjua baba, mfano unapohalibu kitu mama alichokugaramia anakwambia umewah muona baba yako akileta hata sent tano au unauliza mama baba angu yuko wap mama anakujibu alikufa hiv hapa unajenga nn ktk ubongo wako. Kutokana na kukosa michango/malez ya baba hivyo huwa hatuoni umuhimu wa baba
 
Kwa kuongezea viungo tu kwenye hoja yako Yummy:
Binadamu tunazaa miili hatuzai roho,familia moja,baba na mama katika familia yenye 'furaha' lakini watoto wakikua utadhani mmoja alikulia kwa askofu na mwingine kwenye kijiwe cha wavuta bangi, cel a vie mademoiselle Yummy.
 
mkuu kuna wakati unajihisi kama una mapungufu fulani kwa kitendo cha baba kuwa mbali na wewe utotoni? na vipi baba akija sasa hivi na kutaka kujenga uhusiano na wewe,utamkubalia?


Asubiri nifariki kwanza, ili aje kupigania urithi, kama Mzee Kanumba....
 
kwani ni kosa au mtu anapenda kulelewa na mzazi mmoja? jadili tabia ya mtu binafsi na sio ooh kalelewa na mzazi mmoja...HAIHUU!
 
pole sn, tutolee macho tulipojikwaa sio tulipoangukia.U NEVER KNOW!
 
mkuu kuna wakati unajihisi kama una mapungufu fulani kwa kitendo cha baba kuwa mbali na wewe utotoni? na vipi baba akija sasa hivi na kutaka kujenga uhusiano na wewe,utamkubalia?

Si mpaka amjue huyo baba'ke. Watoto wa uzinzi na wanaolelewa na mama pekee wengi wao huwa hawajui baba zao au huwa wanabambikiwa/singiziwa baba.

Soma zaidi: https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/363031-nusu-ya-wako-watoto-ni-wa-kusingiziwa.html

Takwim:Asilimia 48.3 Ya watoto waliozaliwa sio watoto wa baba halisi.wengi wamebambikiwa - Salma Msangi
 
Kosa si kosa, kosa nikurudia kosa,tuhangaike na tulipojikwaa sio tulipoangukia. U NEVER KNOW!
 
Tabia ya asili ya mtu inatokana na wazazi wote wawili kutokana na jenetiki zao..
But tabia za ziada zinatokana na malezi pamoja na mazingira.

Kwahiyo hakuna fomula maalum ya kutambua tabia ya watu/mtu fulani..
Kumbuka;
Binadamu hawafanani kitabia...
 
kiukweli hali ya kulelewa na mzazi mmoja tu inauma sana,,mm mwenyewe sometime nilikuwa natamani sana kuita baba lakini ndo hivyo tena,,namshukuru mama yangu kwa kunilea na kunipa kile kilichokuwa ndani ya uwezo wake mpaka leo ninasoma masterz yangu,,ki ukweli sina mapenzi na baba hata kidogo,,simchukii ila simpendi,,
 

Huwa nakukubali siku zote, ushauri murua huu. Ubarikiwe sana. Siku zote ushinde ubaya kwa wema. Haijalishi ni katika mzaingira ya namna gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…