Mwanaume Hana Moods

Aseeee!!
Duh!!
 
Hapo tu ndio kina mama huwa mnachemsha. Mtu akishakuwa kimya akitafakari mambo ya familia basi inakuwa ishu. Mara baba fulani unaumwa? hapana. Umekasirika? hapana. Mbona uko kimya? Kuna mambo natafakari? Mambo gani unatafakari? naomba muda ni tafakari mwenyewe nitakujulisha? Au nimekuudhi? Hapana? Sasa kwa nini hutaki kuniambia kinachokufanya uwaze? nimesema naomba muda nitafakari wewe hauhusiki? Kwa nini sihusiki wakati mimi ni mke wako? Au huniamini ndio maana hutaki kuniambia kinachokupa mawazo? Bwana eee *&@##...........**&^^^&. Yaani ni maswali kwenda mbele mpaka sasa inakuwa kero.

Ushauri wa bure kwa kina mama: Lazima ujue behaviour ya mwanaume. Sisi hatuna kawaida ya kumweleza kila mtu yanayotusibu na ni mara chache sana kukuta mwanaume anaongea mambo ya ndani kwake kwa marafiki ama kwenye vijiwe/bar. Na kabla hujaanza kimweleza mtu inabidi utafakari kama kwa kufanya hivyo unajenga au kubomoa. Na kuna vitu vingi huwa tunaamua kuvificha vifuani kwa maslahi ya wanawake zetu na watoto. Hivyo ukiona mwanaume yuko kimya anawaza au kutafakari mpe muda amalize mambo yake sio unaanza kuingilia kati kwa maswali na kutaka kugeuza suala zima kuwa ni kati yako na yeye. Siyo kila mara anapowaza ina maana ni wewe ndiye chanzo. Kuna vyanzo vingi vya stress na wakati mwingine siyo busara sana kuvisema.
 
Dena Amsi, hujambo dada yangu? mimi nataka kujua tu sababu hapa ulipata ushauli wa kila aina. Je mwanaume kasharudisha mood? sasa hivi mambo yanaendeleaje? Mia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…