Mwanaume Hana Moods

Dah.......hapo kwenye red nyamayao unabaki kujiuliza hivi ananisemaje kwa mama! Maana mpaka aambiwe aje apumzike ndo kusema mke umeshindwa kumpumzisha eh. Kaazi kweli kweli

Bi dada hapo kwenye blue nimecheka hadi machozi!! mwe mie nilikondaje halafu anapita barabarani akinisema kwa wenzie eti nina ukimwi jamani!! Asa nkiwa nao mie, yeye ndo mzima?! Ila nimemsamehe kutoka rohoni kwani hakuwa anajitambua na bahati yake mbaya kuwa ndo nshakuwa Ex.
so my dear...haya matatizo cjui ya kununiwa,cjui kasusa kula ni wengine 2nayaona ya kawaida sana...

Mweleze da mkubwa maana naona Dena anaumia haswa!
 
Kabla sijamwaga mapointi yangu yaliyonifanya kutunukiwa digrii ya heshima na chuo cha ustawi wa jamii,

Naomba kwanza kuuliza:

Eti "mood" ni mkoa ulioko bara au visiwani?
 
so my dear...haya matatizo cjui ya kununiwa,cjui kasusa kula ni wengine 2nayaona ya kawaida sana...

Kwa kweli kila siku nikikukosa nakosa amani si unaona stress zinapungua sasa kwa haya maneno yako dear (Hlafu umepotea sana na wewe siku hizi)
 
dena nadhani kuna jambo ambalo linaweza kuwa linamsumbua au kumsuta hivyo anashindwa kujiamini na kuongea na wewe.. mara wanaume kuna maaamuzi wanaweza kuyafanya nje ya mipango yake na mkewe na akajikuta amepata hasara au ameharibu sasa anakosa ujasiri wa kukuelewesha hivyo anakuwa na hasira na tabia za ajabu ajabu kama ukaidi na kiburi.

cha kufanya, kuna mambo au vitu ambavyo huwa vinamfanya awe na furaha jaribu kumfanyia kama chakula au movie au vipindi kwenye TV.. naamini kwa muda ulioishi nae utakuwa unamwelewa ni wakati gani ana furaha , huzuni, mawazo, nk .. hivyo nenda nae taratibu maana anaweza akakugeuzia wewe kibao kama ndo tatizo
 
Kabla sijamwaga mapointi yangu yaliyonifanya kutunukiwa digrii ya heshima na chuo cha ustawi wa jamii,

Naomba kwanza kuuliza:

Eti "mood" ni mkoa ulioko bara au visiwani?
Yaani Babu una degree ya chuo cha Ustawi ilhali ramani ya nchi yako huijui!!!
 
Kabla sijamwaga mapointi yangu yaliyonifanya kutunukiwa digrii ya heshima na chuo cha ustawi wa jamii,

Naomba kwanza kuuliza:

Eti "mood" ni mkoa ulioko bara au visiwani?
Aspriniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Kama yupo tuu down mpotezee kwa muda. Wala usihangaike kujaribu kurudisha mood yake. Huu ni wakati wa wewe kwenda shopping sio kumbembeleza. Kama ni moods tuu na hakuna kingine zaidi he will come back. Ndio wanaume walivyo. Kumbuka while women are from Venus, men are from Mars.
 

Umenena vyema nitaufuata ushauri wako..............
 

Thank you EMT..............
 
Reactions: EMT
dena jambo jingine inawezekana kuna jambo ambalo unamkera au linafanyika hapo nyumbani na anashindwa aanzeje kulisema labda linaweza kukukera au likaleta kutokuelewana zaidi hivyo anajenga chuki juu yako.. cha kufanya kama nawe unaogopa kukaa nae na kuongea tumia watoto au unaweza kupanga out moja kwa ajili ya mazungumzo nje ya nyumbani .. but usimweleze yeye anakukosea nini ila jaribu kumwelezea malengo na maisha ya mbele au kuwa na plan fulani ambayo ataona ni ya maendeleo kwake
 

"nilikuwa na2mia nae kinga so nilivyojua hivyo ikanibidi 2 nitengane nae"...gosh! huyu wako mbona alipitiliza hivi jamani, mwanaume mkamilifu haongelei mambo ya mpenzi wake hata kidunchu kwa washkaji, pole ndao! hapo ukirudi mie nakuja kukutoa kwa mangumi.....
 
Dena kwani ni muda gani sasa yuko katika hali hii?
Na ukijaribu kumuuliza kwa upole ni maswaiba gani yamemkuta anakaa kimya hajibu ...?
 
Samahani kwa kuchakachua sredi.........

Naomba kukuuliza DA na MJ1

Hiyo mood mnayozungumzia hapa iko kwenye kikojoleo cha mme wake Dena au kwenye wallet?

Vyote ndugu yangu..........
 
nionavyo mimi kuna kitu umemfanya. hataki kukuuliza labda anafanya uchunguzi sasa kinamkaba kooni. jichunguze, jirekebishe. tulia tu endelea kumhudumua kwa akili, busara na unyenyekevu. atakisema tu kitu hicho.
 


Dah nimeshajaribu hayo mambo lakini wapi tena nikutumia watoto ndo balaa anawaambia ndo mama yenu kawatuma sio..........
 
Dena kwani ni muda gani sasa yuko katika hali hii?
Na ukijaribu kumuuliza kwa upole ni maswaiba gani yamemkuta anakaa kimya hajibu ...?

Mama wa Kwanza we acha tuuuu ni muda kama wiki tatu hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…