Ventas Malack
Member
- Jul 18, 2022
- 5
- 1
Mwanamke ni taswira na dira ya familia na jamii kiujumla kwakuwa ni mama pia ni mwenye nguvu anategemewa kama ilivyoelezewa katika vitabu vingi vya dini, ambapo hivi hueleza kuwa mwanamke ametoka kwenye ubavu wa mwanaume hivyo humkamilisha mwanaume na familia yake.
Kiujumla mwanamke ni uzima wa mwanaume na mwanaume ni jukumu la mwanamke wake.Hivyo basi ukikosea Mwanamke wa kuoa itakuwa ni hasara kubwa utaharibu kesho yako na mfumo mzma wa maisha yako Kwakuwa mwanamke ndiyo nguvu ya mwanaume, jasiri na mtunzaji wa familia pia ni tegemeo la familia na mwalimu wa watoto na familia yake, mlinzi wa familia, chanzo cha baraka, hivyo kuoa mke mwema ndiyo jambo la mafanikio zaidi kwa mwanaume kukosea huweza kuwa ni majuto ya maisha yote mana ukioa mke asiye mwema kwako ni hatari kwakuwa ndoa hubadili historia na maisha kabisa.
Kupitia tafiti zangu ndogondogo na kusoma vitabu kadhaa vya mahusiano nimefanikiwa kupata tabia tofauti tofauti za mke bora ambazo ni chachu kubwa ya mafanikio ya mwanaume kimahusiano na kimaisha kiujumla ambazo ni;
1: Mke mwema Huaminika yaani hujitahidi kwa kila namna ili kuaminika na mumewe katika mambo yote ambapo hii pia humpa nafasi ya kufanya vyema katika ndoa na kusababisha maendeleo katika familia siku zote imani ndiyo uhai wa mahusiano bila hiyo huvunjika mapema sana kwa kukosekana kwa imani ambapo anapoaminika humfanya mwanaume kupambana kwa nguvu zote kwa kuwa hana hofu juu ya mkee aliyemuacha nyumbani.
2: Si tegemezi wala Mnyonyaji, Tafadhali hapatuelewane vizuri kiuhalisia mwanaume ana jukumu la Kumtunza na kutafuta kwaajili ya mwanamke wake na kuhakikisha anapata mahitaji lakini siyo mwanamke kumfanya mume kama mradi au biashara fulani au kuolewa na mtu ni kwaajili ya kupata sifa kuwa kaolewa na jamaa aliye na uchumi mzuri na pesa hivyo ni muhimu mwanamke kuwa si tegemezi ajitahidi hata atoe mawazo kwa mume kwaajili ya kuendeleza uchumi wa familia na siyo kumnyonya kiuchumi na kutumia tu pesa hii huchosha sana na kurudisha nyuma wanaume.
3: Ana Uvumilivu mkubwa, ili aitwe Mke bora na mwema lazima awe na uwezo mkubwa wa kuvumila na kuwa na subira katika ndoa yake hasa pale ambapo mume anayumba kiuchumi, kiafya na katika mambo mengine, hii ni nguzo kubwa sana katika ndoa na mahusiano maana mwanamke akikosa kiwango cha uvumilivu huweza sababisha matatizo sana katika ndoa ikiwemo usaliti na gomvi mara kwa mara hivyo mke mwema ni yule anayekuwa mvumilivu sana na mwenye upendo ili kumpa nafasi mwanaume ya kupambania mabadiliko na maendeleo.
4: Mlinzi, lazima mwanamke apambanie usalama wa mume na familia yake katika afya,saikolojia na mengineyo ni kweli mwanamke hawezi kupigana na majambazi au wezi lakini kuna mambo ambayo akiyafanya familia yake huwa salama ambapo hawezi kumuumiza mume wake, kumtendea ubaya pia kumchafua mumewe ambapo hii humpa nafasi mwanaume wanawake wengi hawajui mume akipata stress hata kidogo kidogo huwa na mfadhaiko na msonono mkubwa kuliko hata wanawake ambayo ni hatari kwa mahusiano yenu na hata maendeleo ya familia.
5: Ana Utii sana ,wanaume hawahitaji kupendwa tu na wake zao ila wanaume wengi hupendelea heshima kutoka kwa wake zao hivyo mke mwema ni yule ambaye ana heshima pia ni mtii kwa mume bila kujali hali yake ya kiuchumi, kijamii na hata kimaumbile uwepo wa hili humpa morali mwanaume kumpenda sana mke wake huyo kwakuwa tu ni mtii, mwanamke anatakiwa kujishusha na kufanya maamuzi kwa busara wakati mwingine hata akikosewa na mumewe asipaze sauti sanaa humfanya mwanaume aone haheshimiki na kuona ndoa yake si kitu.
6: Siyo msaliti, ili aitwe mke mwema lazima awe siyo mtu msaliti kwa mume kwakuwa hiyo hulinda heshima ya mumewe na pia afya ya mumewe, watoto ambapo mke huyu mara nyingi hujiepusha mbali na wanaume wengine ili kuzuia usaliti.
7: Ana upendo wa kweli, mke mwema anakuwa na upendo mzito kwa mume, watoto, familia ya mumewe na familia yake pia ambapo hii chanzo kikubwa cha utulivu na amani katika familia endapo mwanamke atakosa upendo hata kupokea na kufikiwa na wageni nyumbani huwa ni ngumu maana watakua wanaogopa kufika hapo hivyo akiwa na upendo ni faida kwa familia na ni chanzo cha baraka zako pia mshikilie.
8: Anatunza siri, mke mwema anatakiwa kuwa na tabia ya kutunza siri za familia, mumewe na awe na uwezo wa kuyatunza yanayojiri kwenye familia yake kwa kuwa akiwa mwepesi kuyatoa nje ni aibu kwa familia na mumewe hivyo basi aweze kutunza siri ili kuafanikisha mipango ya familia yake mara nying si wote wanaosikia mambo kuhusu wewe na familia yako watafurahi hivyo akiwa mtunza siri ni faida sanaaa.
9: Huwa hana Tamaa, mke mwema huwa hana tamaa hasa ya vitu ambavyo siyo vya tabaka lake kwakuwa akiwa na tamaa sana ataweza kusaliti au kumtendea ubaya mume hivyo basi ukipata mwanamke ambaye hatamani makubwa ana ridhika na hali zote na yale mliyo nauo basi mshike sana kwa kuwa taswira yako ya kesho ni njema utapokuwa naye.
Kaka kama ukiona mwanamke ambaye upo nae yuko na sifa na tabia kama hizi fanya maamuzi mapema umuoe ila kama kwa bahati mbaya hana jaribu kumtengeneza kwa muda ila ukishindwa bora umuache halafu tafuta mwingine maana. . . . . . . . . . . HERI NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI.
By Ventas MalackView attachment 2350046View attachment 2350047

Upvote
1