Mwanaume Kujiamini ni Silaha Tosha Kwenye Mahusiano

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
38,342
Reaction score
88,625
Wanaume huwa mnaamini mwanamke mwenye muonekano fulani hawezi kuwa na wewe. Kwa mfano mwenye kazi nzuri kukuzidi au mwenye mvuto unaohisi wewe humfai. Mnachokosea ni kwamba mwanamke akikupenda hata uwe muokopa makopo atakukubalia. Ukiwa unapiga sound usianze kutumia maneno ooh najua mimi sio level yako we mzuri sana wewe una kipato kunizidi wewe this wewe that blah blah. Nenda kwenye point sio kuanza kujilalamisha uonewe huruma. Mwanaume ukijiamini hata uweje utapata mwanamke unaemtaka. Kazi yako au muonekano wako hauhusiani na mapenzi yako.
Natamani huyu kaka alonipigia simu saa hizi asome hapa maana hata kama nilipanga kumkubali basi tena keshanikosa.
 
Akikuchoka hajakupenda. Na sawa huna pesa au mwanamke mzuri kwanini ulete hayo wakati unatongoza? Ili uonewe huruma au kitu gani?
[emoji23][emoji23][emoji23]Sio suala la kuleta hayo masuala ya kulia lia ili uonewe huruma

uhalisia wa mambo ndiyo utakao kufanya uchokwe na huyo mwanamke

kwa asilimia kubwa wanawake wazuri huwa wanahitaji kugharamiwa ukiwa upo nyuma nyuma kwa masuala ya kucare ndiyo hapo wengine wanakuzidi kete

Ni bora upate unayeendana nae tu hao wengine ni stress
 
Basi kama unajua sio level yako unamtongoza wa nini? Ina maana huoni unaolingana nao? Ndo yale yale mtu anatongoza mwanamke kibonge halafu anaanza kumwambia apungue wakati kuna wembamba kibao kawaacha
 
Jamani eti nakutana na mwanamke siku ya kwanza naanza tu kumwambia "nakupenda" bila hata kumsifia sifia jinsi alivyo eti kwa kuwa umesema niende kwenye point hiyo hapana

ngoja nika google nipate muongozo " how to start conversation with beautful girl ntapata nyingi tuu
 
nakupenda from bottom of my heart πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚ umekubali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…