Loading failed
JF-Expert Member
- Sep 14, 2023
- 2,603
- 7,501
Daniel Wanyeki Gachoka mwenye umri wa miaka 59 kutoka Kenya ameachiwa huru baada ya kukaa gerezani kwa miaka 17 na baadae kugundulika kuwa alifungwa kimakosa
Wanyeki alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela katika Gereza la Kamiti Maximum Security kwa madai ya kuwanajisi binti zake wawili wa umri mdogo.
Hata hivyo, wiki jana, Mahakama Kuu ya Kiambu ilibatilisha hukumu yake, ikitoa uamuzi kwamba alikuwa amehukumiwa kimakosa.
Uamuzi wa mahakama ulifuatia mabadiliko makubwa ambapo binti za Wanyeki, ambao sasa ni watu wazima, walifichua kuwa walilazimishwa kumshtaki baba yao kwa uwongo mwaka wa 2007.
Wanawake hao wawili walitoa ushahidi mahakamani kwamba walikuwa wameshinikizwa na bibi yao kutoa ushahidi wa uongo dhidi ya Wanyeki ambapo mahakama ilikubaliana na ushahidi huo
Hata hivyo Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) imependekeza Wanyeki asubiri hadi Desemba 4 mwaka huu ili kesi hiyo ifanyiwe ukaguzi na kuona kama ni kweli anastahili kuachiwa huru