Mwanaume mzima unakula chipsi kuku unaacha dona na mihogo

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
14,540
Reaction score
30,875
Mungu tunusuru wanaume tumebaki wachache sana, foleni kubwa ya wadada wanasubiri na kuweka odder za chips Yai na kuku ghafla unakuta likidume lipo katikati ya wanawake na lenyewe linasubili chipsi [emoji848].

Mkigongewa wake zenu mnafoka nakati mnayataka wenyewe, mwanaume kula ugali wa dona na samaki wakuchemsha, gonga mihogo mibichi, nazi na karanga wa kutosha sio kula bugger na piza sijui bufee magonjwa hayooo unauwa nguvu zako za kiume.

Wanaume tuache kula vya kula vya kike.
 

Me naona matunda muhimu sana kama unaweza yapata mda wote
Dona miogo isikuogopeshe kutokula
 
Wewe pia acha kuwaza ngono. Ungewaelewesha watu wale ivyo vyakula kwa afya kiujumla ila umefocus kwenye ngono tu, unaweza ukawa na ufanisi kwenye tendo na bado ukawa na maradhi mengine ya kiafya
 
Akimaliza Kula chips anaagizia na Energy Vijana wamelegea kuliko hata wazee.
 
Mkuu tulizaliwa tukakaririshwa hivyo sikatai.

Lakini tuliposoma na kuelimika, tukaja gundua kuwa kumbe mahindi (maize meal), yawe ni unga wa sembe ama dona ndiyo chakula chenye thamani ya chini kabisa kuliko vyote katika vyakula vya mazao ya nafaka!

"Food value" ya mahindi hailingani na ngano, mchele, mtama ama uwele.

Na pia hauwezi kulinganisha na vyakula vya mizizi kama mihogo na viazi.

Kwa wazungu huko, mazao ya mahindi ni chakula cha mifugo kuanzia majani na mbegu zake.

Kabla ulimwengu haujastaarabika, kwao mahindi kilikuwa pia ni chakula cha watumwa.

Tukitaka kusifia milo, basi tuchunguze kwanza ni chakula gani tunachoweza kutoka nacho hadharani na kujikisifia kutumia.

Mi nadhani mtu anayekula wali ama chapati ana gain more energy kuliko anayekula ugali.

Ugali kiuhalisia ni chakula cha chini sana na hakina thamani yoyote katika afya ya binadamu.

Kuna baadhi ya nchi hawaelewi kabisa stori za kitu kinachoitwa ugali na wako strong sana ki afya na wanatuzidi wala ugali!
 
Unakutana na mwanaume mtu mzima na midevu yake anamwambia muuza chipsi "mayai yasikauke Sana alafu weka mayonaizi na soseji mbili" naishia kujiuliza hivi huyu akitoka hapa anawezaje kuchakata mbususu kwa mkewe?

Food industry ni moja ya silaha hatari Sana inayomwangamiza mwanaume kimya kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…