mtakatifu wa 2
Member
- Apr 15, 2022
- 22
- 45
Baada ya njaa kali nimejikuta nikifanya uchunguzi na kugundua uhusiano uliokuwepo kati ya mwanaume na jua, na mwanamke na mwezi katika maisha ya kila siku.
Mwanaume na mwanamke kila mmoja ana aina fulani ya nguvu ya asili. Endapo Tukifuata msingi huo, kwa kawaida tutajisikia furaha, utulivu, usalama, katika mahusiano yetu na vilevile amani ya moyo itastawi. Kwa mfano, nguvu ya mwanaume(JUA). Anang'ara, anawajibika kwa familia yake, mlinzi wa familia, anasimamia ukuaji wa uchumi wa familia, mchapakazi. Mwanaume akitimiza sifa izo anajisikia furaha na kuridhika kwasababu anaishi kulingana na asili yake.
Tofauti na nguvu ya mwanamke(MWEZI). Anasaidia kila mtu "kupoa" katika kivuli chake baada ya siku ndefu na yenye uchovu. Mwezi huleta amani na utulivu, uleta faraja kwenye huzuni, uleta matumaini kwenye kukata tamaa.
Je ni wangapi kati yetu wamegundua ili na wanaishi kulingana na asili zao? Je ni kwanini hatuna furaha,je kwanini tunachoshwa na maisha ya familia? rejea mfano wa Bundi anaona vizuri usiku kuliko mchana. Japo anaweza fanya mawindo mchana ila haitakuwa rahisi kama angeyafanya usiku, akijaribu kufanya ivyo mara nyingi anaweza akafa kabla ya wakati wake.
Je kwetu sisi ni tofauti tunapotaka kuishi tofauti na nguvu zetu za asili? wengi wetu tumesahau majukumu ya asili.katika dunia ya sasa, Je mwanamke apambane kupata mafanikio binafsi, na mwanaume ajihudumie mwenyewe? kwamba mwanamke kwa akili zake binafsi adhihilishie kwa dunia anaweza kufanya chochote.
Je inawezekana kuwa JUA na MWEZI kwa wakati mmoja? je 50/50 inawezekana? je kwanamna gani nusu ya siku huishi kama mwanaume na nusu nyingine kama mwanamke? mnafikiri itawezekanaje?
Nakubaliana na atakayesema INAWEZEKANA. Je maumivu yake ni kiasi gani na yatadumu kwa mda gani?
ukweli ni kwamba kati ya nguvu izi mbili (jua na mwezi) moja ni kubwa kuliko nyingine. Endapo mmoja atabadilisha nguvu yake ya asili je nini kinaweza tokea? Mwanamke akibadili asili yake nakulazimisha nguvu ya JUA. Muda mwingine inawezafanya kazi vizuri tu, baada ya mda ataanza kuhisi homa zisizo eleweka, 24/7 tiredness, kutojaliwa(apathy), mwisho kansa na msongo wa mawazo.
je kila mtu anatimiza majukumu yake ya awali, au tunaishia kulaumu kila kitu au watu kwanini tunaugua sana siku izi?
Kwa uzoefu wangu mdogo nimekutana na baadhi ya "wanawake JUA" wengiwao wamefanikiwa tena sana tu,ila hawana furaha. Wanajaribu kuonesha kwa jamii kwamba wanafuraha, lakini sio kweli! Kiuhalisia wanamajonzi makubwa nafsini mwao na wamechoshwa kufanya vitu pekeyao bila usaidizi. Wanatamani wapate mkono wa usaidizi, lakini kadri wanapo uhitaji mkono huo ndivyo unavozidi kwenda mbali zaidi, hii inawaacha na majonzi makubwa kwenye maisha yao.
Je ni kwanamna gani nguvu izi mbili zinashirikiana JUA na mwezi, fuatilia mifano ya muunganiko wa familia izi:
1.JUA&MWEZI
Mwanaume ananguvu ya jua.
mwanamke ananguvu ya mwezi.
mwanaume anatimiza majukumu yake vyema kwa mkewe na watoto. mwanamke anajali na anahakikisha utulivu wa familia yake.anamsikiliza mumewe.mwanaume ndio kiongozi wa familia.familia hii inafuraha sana kwani kila mmoja anaishi kulingana na asili yake.katika familia hii watoto wanalelewa katika malezi sahihi kwani wanajifunza kipi ni sahihi kulingana na jinsia zao.
2. JUA-JUA
mwanaume ananguvu ya jua.
mwanamke ananguvu ya jua.
familia hii ipo kwenye gonvi na mafarakano kila wakati.kila mmoja anataka uongozi wa familia,wanashindana kutimiza majukumu ya msingi,hii mwisho hupelekea wote kuchoka sana,mwanaume anamaliza nguvu kushindana na mkewe ilihali alitakiwa kuzitumia kupambana na mitaa kutafuta ridhiki ya familia.
3. MWEZI-MWEZI.
Mwanaume ananguvu ya mwezi.
Mwanamke ananguvu ya mwezi.
Majukumu ya familia yanamuelemea mwanamke,mwanaume hana matarajio yeyote kwenye mahusiano ayo, lawama zitatokea kila kukicha kwani mmoja atamlaumu mwenzake katika kila litakalotokea kwa kutotimiza majukumu yake katika familia.
Je ni upande upi umezidi kukiuka majukumu yake ya asili,na unahisi kwanini unafanya ivyo, na nini kifanyike ili kila mmoja aishi kilingana na nguvu yake ya asili?

Upvote
0