Mwanaume ni kiumbe cha pekee sana hapa Duniani, kuliko kiumbe chochot

Mwanaume ni kiumbe cha pekee sana hapa Duniani, kuliko kiumbe chochot

green rajab

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
12,387
Reaction score
39,119
*Mwanaume_ni_nani...!!!?*

Mwanaume ni kiumbe cha pekee sana hapa Duniani, kuliko kiumbe chochote...!!

Mwanaume anaweza kumuacha mwanamke aliyemfumania kisha akaoa mwanamke aliyeachwa kwa kosa la kufumaniwa...!!

Najua ipo humu ila nimependa hiyo mistari [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mkuu ww ni mwanaume?
*Mwanaume_ni_nani...!!!?*

Mwanaume ni kiumbe cha pekee sana hapa Duniani, kuliko kiumbe chochote...!!

Mwanaume anaweza kumuacha mwanamke aliyemfumania kisha akaoa mwanamke aliyeachwa kwa kosa la kufumaniwa...!!

Mwanaume anaweza kumkataa mtoto wake halali kabisa kisha akasingiziwa mtoto wa mwanaume mwingine na akakubali...!!!

Mwanaume ni kiumbe cha pekee ambaye anatafuta hela kwa jasho na nguvu kwa ajili ya mwanamke...!!!

Mwanaume ni kiumbe cha pekee ambaye anaweza kujiua kisa tu amekataliwa na mwanamke..!!

Mwanaume anaweza kupanga mipango kichwani, ambayo inaweza kudumu kichwani mwake hata miaka kumi...!!

Mwanaume yupo radhi hata kulala na njaa, ili mladi tu atimize adhima yake...!

Mwanaume kweli ni wa ajabu sana, anaweza kufuta kwenye kiti anachotaka kukaa, ilihali boxer aliyovaa hajaifua wiki 2..!!

Mwanaume anaweza akawa na wanawake hata 3, lakini mkewe wa ndoa asijue hata siku moja..!!

Mwanaume anaweza kuishi na mke wa ndoa zaidi ya miaka kumi Wakiwa wamepanga, lakini ana hawara amemjengea nyumba safi kabisa..!!

Mwanaume anaweza kuwa na heshima nchi nzima, mkoa mzima, Mtaani kote, lakini nyumbani kwa mkewe, anaonekana boya kabisa, na deki anapigishwa, na vyombo anaosha..!!

Mwanaume anaweza chuma mali na mkewe, na mwisho akamwachia mkewe zote, Na akaanza upya...!!

Mwanaume anaweza akawa na kazi nzuri lakini akawa anaishi kwa mwanamke akamjengea, akamfungulia biashara, ila akifukuzwa tu kazi anakosa pa kuishi na mwanamke nae anamfukuza....!!!

Kama hujui mwanaume akili yake inawaza mapenzi kwa asimilia kubwa kuliko mwanamke...!!!

Kama hujui pia wanaume wengi wanateseka kwenye mahusiano lakini wanajifariji kwenye pombe...!!

*Ndio maana tunakufa mapema....!!!*
 
Usipende kutumia neno 'mwanaume' au 'wanaume' kwenye maelezo yako, japo wote ni binadamu lakini tumetofautiana attitude na akili, tumia neno "baadhi ya wanaume" sio wanaume,
 
Mwanaume anaweza kumnyima mwanae Wa kumzaa ada ya shule, akaenda kusomesha watoto watano Wa mwanamme mwingine kwa mchepuko wake
Yaani kawaida sana hiyo kitu nyumbani Dagaa kwa mchepuko Sato
 
Back
Top Bottom