Mwanaume ukiwa huna pesa unakosa nguvu ya maamuzi kwa mkeo

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Nguvu ya mwanaume siku zote ni uchumi/kipato. Kipato kinapokuwa chini hata nguvu pia ya kusimamia familia pamoja na mkewe hushuka. Inapotokea mkewe au mpenzie kumzidi kipato au cheo, hapo pia nguvu ya mwanaume huathiriwa.

Mwanaume anakuwa hana nguvu ya kumuamrisha au kumuelekeza mkewe. Matokeo yake mmewe inabidi aisimamie ile nafasi ya mwanamke kwa kuwa mpole pamoja na kufuata maelekezo ya mkewe.

Nilishashuhudia sehemu fulani, mume ni dereva na mke ni afisa, kilichotokea mumewe alikuja kufa kwa msongo wa mawazo, na alipougua alikuja kuuguzwa na ndugu zake (mwanaume) huku mkewe akiwa masafa akila bata na wale ambao anafanana nao kiuchumi.

Ikitokea kwa bahati mbaya ukaangukia katika uhusiano wa namna hii, ni bora utafute kifaa cha pembeni ili uwe unapooza machungu pale mambo yatakapokugeukia. Ni vigumu binadamu kuacha asili aliyoumbwa nayo, mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho, sasa kama mwanamke ndio ale kwa jasho hapo lazima baharia aishi kwa uchungu.
 
Mimi bado ninaamini kuwa mwanaume anapokuwa amezidiwa na mwanamke kipato swala la kujishusha na kumpa mwanamke madaraka akutawale ni udhaifu tu wa mwanaume mwenyewe.Na hili linatokea pale unapotaka akutawale ili uendelee kupata neema ya mali zake au utajiri wake.Ushauri wangu ni kuwa usikubali kutawaliwa na mwanamke hasa ukiwa kwenye mahusiano,swala la utawala Mungu alituachia sisi wanaume ndani ya nyumba zetu,hata kama atakuwa ni waziri,uwaziri wake unaishia mlangoni anapoingia ndani,yeye ni wa kuwa chini ya mwanaume tu,ukiona una mwanamke anapingana na hiyo hali ujuwe huyo hakufai na ukiendelea kuruhusu hiyo hali ya kutawaliwa jua kuwa uhai wako unauweka rehani kwa maradhi,utakufa mapema kwa magonjwa ya kusononeka utamuacha mwenzako anaendelea kula maisha...
 
Mwanaume asiyekuwa na pesa anatumia mabavu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni wanaume wachache wasio na uwezo wanafurahia maisha ya ndoa, wengi wao wanapitia stress.
Ni kuomba tu Mungu akujalie mwanaume kama hujaoa basi upate mke mwema ambaye atakuheshimu na kukupenda kwa kiasi kile kile hata siku maisha yakiyumba.
 
Mkeo akileta nyodo za kipato ondoka nyumbani nenda katafute, usiache kuhudumia familia kwa kidogo unachopata huko huko ulipo. Hakikisha unapata hamasa ya kufanya kazi zaidi.
Unaweza ukafanya kazi zaidi na bado kipato kikawa tofauti, ni sawa na injini ya bajaji uweke kwenye fuso, kitakachotokea ni injini kuungua tu
 
Mimi bado ninaamini kuwa mwanaume anapokuwa amezidiwa na mwanamke kipato swala la kujishusha na kumpa mwanamke madaraka akutawale ni udhaifu tu wa mwanaume mwenyewe.Na hili linatokea pale unapotaka akutawale ili uendelee kupata neema ya mali zake au utajiri wake.Ushauri wangu ni kuwa usikubali kutawaliwa na mwanamke hasa ukiwa kwenye mahusiano,swala la utawala Mungu alituachia sisi wanaume ndani ya nyumba zetu,hata kama atakuwa ni waziri,uwaziri wake unaishia mlangoni anapoingia ndani,yeye ni wa kuwa chini ya mwanaume tu,ukiona una mwanamke anapingana na hiyo hali ujuwe huyo hakufai na ukiendelea kuruhusu hiyo hali ya kutawaliwa jua kuwa uhai wako unauweka rehani kwa maradhi,utakufa mapema kwa magonjwa ya kusononeka utamuacha mwenzako anaendelea kula maisha...
Na wengi huwa wana msongo wa mawazo
 
Mwanaume asiyekuwa na pesa anatumia mabavu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ha ha ha anatumia mabavu kwenye nini? na anaweza akatumia mabavu na vyote akanyimwa, njia pekee ni kutafuta unayemzidi kipato; tofauti na hapo tunaigiza, kwa nje tutaona mko poa ila uhalisia unaujua wewe mwenyewe kwenye nafsi yako unavyoumia.
 
Ni wanaume wachache wasio na uwezo wanafurahia maisha ya ndoa, wengi wao wanapitia stress.
Ni kuomba tu Mungu akujalie mwanaume kama hujaoa basi upate mke mwema ambaye atakuheshimu na kukupenda kwa kiasi kile kile hata siku maisha yakiyumba.
Zamani watu walikuwa wakipendelea kuoa walimu, manesi n.k yaani zile kada ambazo hazimkuzi mtu kupata mapato makubwa, na lengo ni kupata utulivu ndani ya familia.
 
Ila bado wengine waliumia, tabia ya mtu ni kitu binafsi haihusiani na kazi au cheo chake.
Kuna wanaume wameoa wamama wa nyumbani ambao hawana kipato chochote kusema kinawapa jeuri, ila ile stress wanapata huko ndani wanatamani wahame nyumba zao wenyewe.
 
Wanamna hiyo ni rahisi kuwamudu kama umewazidi kipato, na unaweza kujifariji utapata mwingine, ila aliyekuzidi kipato ikatokea mmetofautiana mwanaume anakuwa kama mbwa koko aliyerudisha mkia nyuma na kukimbia, hata mkiachana yeye bado ataendelea kuwa na maisha mazuri zaidi. Pale mwanaume anakuwa kama alikuwa mnyonyaji.
 
mkuu mbona wapo wengi tu wenye vipato vikubwa wanaendeshwa na kila kitu na wake zao, je hawa nao tuwaweke kundi gani?

kutawaliwa na ke katika ndoa/mahusiano hakuna uhusiano wowote nakuzidiwa kipato bt hii inatokana na hulka ya asili ya mwenza wako kama anapenda kutawala/kutawaliwa katika mahusiano ndo maana kuna wenye vipato na wanatawaliwa na wake zao.
 
Hao watakuwa sio wanaume orijino, labda uchakachuzi utakuwa umefanyika
 
Mimi bado ninaamini kuwa mwanaume anapokuwa amezidiwa na mwanamke kipato swala la kujishusha na kumpa mwanamke madaraka akutawale ni udhaifu tu wa mwanaume mwenyewe.Na hili linatokea pale unapotaka akutawale ili uendelee kupata neema ya mali zake au utajiri wake.Ushauri wangu ni kuwa usikubali kutawaliwa na mwanamke hasa ukiwa kwenye mahusiano,swala la utawala Mungu alituachia sisi wanaume ndani ya nyumba zetu,hata kama atakuwa ni waziri,uwaziri wake unaishia mlangoni anapoingia ndani,yeye ni wa kuwa chini ya mwanaume tu,ukiona una mwanamke anapingana na hiyo hali ujuwe huyo hakufai na ukiendelea kuruhusu hiyo hali ya kutawaliwa jua kuwa uhai wako unauweka rehani kwa maradhi,utakufa mapema kwa magonjwa ya kusononeka utamuacha mwenzako anaendelea kula maisha...
ili usife mapema wewe simamia majukumu yako kama mume,lisha familia,lipa school fees,rent,na bills zingine zoote na ikiwezekana mpe mkeo hela ya kupendeza hata kama ni mbunge wa ushetu wewe mpe tuu,jifanye huuoni ukuu wake hapo utakuwa na amani....na sio unajitutumua kifua kama kaburi la mtoto halafu huna hata mia na yeye ndio anakulisha,broo lazima ufe nusu karne.
 
Back
Top Bottom