Mwanaume usimuanike mpenzi wako mitandaoni


Unamatatizo Mkuu. Wewe mtu akipost status hata mia moja kwenye simu yake, anatumia MB zake wewe nini kinakuhusu?

Mtu akitumia akauntu yake kumpost mpenzi wake au nyumba yake, au gari lake, hajapost mkeo wala mali yako. Wewe kinachokuuma ni nini kama sio uchawi wenyewΓ© huo?

Ninyi ndio kwenye familia mnavisheria mavimavi havina mbele wala nyuma alafu mkiambiwa mzifafanue mnabaki kubabaika kama majinga. Ni hasara kubwa
 
Ndio ileile concept kuwa Mwanamke WA Ofisini anazagamuliwa huko ofisini hivyo wanaume waoe golikipa.
Yaani kuna Watu wanafikiri kwa namna ya ajabu sana
Mwanamke km hajatulia hata umuwekee ulinzi atapigwa na hao hao walinzi uliomuwekea πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Leo ndio nimegundua kumbe zile mada una copy sehemu sikutegemea kabisa kwa hyo ww kwa akili yako mastaa wote bongo wana akili? Maana naona unatoka nje ya mada zile fasihi kumbe huwa unaandikiwa nilikuwa sijui kumbe ww ni blank kabisaa.
 
Huyo madebe ndyo nani mbona simfahamu
Eti Lamomy huyo debe ndyo nani huko daslama
Ndo ujue watu wako busy kufatilia hata visivyopaswa kufatiliwa bff πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ni muigizaji wa bongo movie ana vimisemo vyake vya kiswahili
 
Wakati unaenda kazini unamuacha mkeo nyumbani unajua huku nyumbani anafanya nini?

Kama unaelimu walau ya kidato cha nne huwezi kuwaza kwa namna uliyowaza.
Tatizo lako unabishana na uhalisia mada ilikuwa wanawake wanaofanya kazi za ofisini sio nyumbani mbona unaruka ruka hutulii kwenye mada moja.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Watibeli wamecharuka leo
 
Wewe hupost mke au huyo mpenzi na Watu wanakamua au mapenzi yanakusumbua na pesa huna. Alafu unawataja Watu ambao huwafikia kwa lolote. Bado Huoni unamatatizo
Pesa sina ila sijawahi kuja kwako kuomba kazi au hela ya kula endelea na fasihi zako za ku copy kwenye vitabu vya shaban Robert.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Kaka chukua maji ushushie 🍸
 
Aloooo! Na DC nae washamchapia?

Ila yule MC kutoka Dodoma mbona yule mke wake ukimuona tu kwenye picha unajua huyu ni mgawaji mzoefu.

Lakini yule msemaji aliyezisemea timu pendwa kwa nyakati tofauti ni kama ana shida kichwani sio kosa lake.
 
Ni ukosefe wa akili na kazi za kufanya huwezi kuta mtu anayejielewa anafanya huo ujinga ndio maana unashinda jf kuleta mada za fasihi hakuna mtu anayejielewa anafanya huo ujinga muda anatoa wapi wa kukesha kwenye upuuzi ambao hauna msaada wowote kwa jamii.
 
Mkuu kwa uelewa wako mtandaoni Watu wanatakiwa wapost jambo gani?

sasa hapo naona unahitaji nifundishe faida na hasara za mtandaoni, right πŸ’


mkikutana mtandaoni na mkawa wachumba na hatimae ndoa, its okay and fine,

otherwise mkikutana kanisani halafu mkakaribisha mtandao kana kwamba ndio furaha yenu na mshauri wenu mkuu wa ndoa basi msijiskie vibaya kuingizwa kwenye list hapo juu, muda muafaka ukifika πŸ’

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Pesa sina ila sijawahi kuja kwako kuomba kazi au hela ya kula endelea na fasihi zako za ku copy kwenye vitabu vya shaban Robert.

Sasa ukiwa huna pesa basi jitahidi uwe na akili Mkuu hata ya kawaida.

Sasa wewe kama kwenda na mkeo tuu Kanisani au kuongozana naye njiani huwezi unaanzaje kuwasema wanaopost huko mitandaoni?

Embu leta hoja yenye maana ili usapoti mada yako.
Kwenye ukoo wenu tuu ninauhakika wapo wanandoa wametalakiana na hata smartphone hawana alafu unakuja kuandika vitu bila hoja zenye nguvu
 
Mi nimekuelewa sana.
Mfano mimi nina mtu wangu, wanaojua ni familia zetu mbili na rafiki wa karibu hivyo hata tukiachana naweze move on kirahisi.
Ila kama niki post Dunia nzima ikajua kesho tukiachana kazi sana ku move on.
Kwanza kila mtu atakuwa anauliza uliza nini kimetokea.
Ukiweka mambo yako mtandaoni jiandae kuandamwa na watu pale yakiharibika
 
Ni maoni yake yaheshimiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…