Mkuu kisayansi vinasaba vyake vinaonesha ana XX...
Labda nikudokeze tu kidogo kwa kuwa tupo jukwaa la utabibu...
Baada ya mimba kutungwa na mtoto kuwa katika hatua za awali za ukuaji, kichanga huwa hakina jinsia.
Baadaye jinsia ya kike ndio huanza kujitokeza hata kama mtoto atakayezaliwa atakuwa mwanaume...
Sasa ili mtoto atokee kuwa mwanaume, sehemu ya clitoris hu-develop na kuwa penis...sehemu ya vulva nayo hu-develop na kutengeneza ngozi ya korodani...vivyo hivyo kwa sehemu nyinginezo.
Yote hayo hutegemeana na information ambayo vinasaba vinakuwa vimebeba ili kuelekeza uumbaji wa maungo na mifumo...
Kuna wakati hutokea kasoro kadha wa kadha katika hiyo process, ndio maana huwa kuna watu huzaliwa jike dume, wengine unakuta wana maumbile ya kike wakati wao ni wanaume n.k