Mwanayanga mwenzangu Jerry Muro hongera huko uliko

Mwanayanga mwenzangu Jerry Muro hongera huko uliko

msela wa mbagala

Senior Member
Joined
Dec 13, 2019
Posts
139
Reaction score
443
Jana ilikua siku nzuri sana kwangu kama shabiki wa yanga, ushindi wetu dhidi ya gwambina kwenye mechi yetu kombe la shirikisho ulikonga nyoyo za wananchi kokote duniani. Ewe mkuu jerry muro mwanayanga mwenzangu nikiri tu kuwa nimekuwa nafurahishwa na namna unavyoiongelea yanga.

licha ya style yako ya upole uongeapo lakini mpangilio mardadi wa usemaji unadhihirisha wazi kuwa ulikosomea taaluma yako ya habari hukuwa unakomalia coursework badala yake ulikuwa unawaelewa vyema walimu wako. namna ulivyoongea ni wazi kuwa wewe mwana yanga mwenzangu kindakindaki ni msomi hasa.

ombi langu kwako kama litakupendeza ukiongelea tena yanga mimi kama mwanayanga natamani ueleze kinagaubaga kuhusu hili jambo ambalo sijalielewa vema. NAOMBA NIKUNONG"ONEZE msisitize ostadh akafundishe vijana pale kariakoo madrasa.

msela wa Mbagala
 
Jamaa anajua kumgusa kipele haji, haji leo analialia tu kutwa nzima
 
Back
Top Bottom