Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Kwa muda mrefu kumekuwepo na imani zinazohusisha ugonjwa wa akili na mwandamo wa Mwezi mchanga. Hata hivyo, kwa sasa imethibitika kuwa, Mwezi mchanga huathiri akili za viumbe hai akiwemo mwanadamu.
Mtaalamu wa Magonjwa ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Said Kaganda alieleza kuwa, Mwezi Mchanga ni kipindi ambacho mwezi mzima huanza kuchomoza baada ya kutoweka kwa siku kadhaa ukiwa mzima (duara). Kutokana na nguvu za uvutano kati ya Dunia na Mwezi, husababisha kupwa na kujaa kwa bahari, pamoja na mawimbi.
Mvutano huo huleta athari kwa viumbe hai kutokana na kuwepo kwa kani mvutano wa elektroniki inayoathiri mwili wa binadamu kutokana na mwili wa binadamu kuumbwa na chaji za umeme kwenye mfumo wa fahamu. Chaji hizo ndizo huathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa hasa mvutano kati ya Dunia na Mwezi.
Dk. Kaganda alieleza kuwa, kipindi hicho cha mwandamo wa mwezi mchanga, tabia za watu (moods) hubadilika lakini wanaoathirika zaidi ni wagonjwa wa akili hasa wa kifafa kwa kuwa, ugonjwa wao (kifafa) umetokana na kuathirika kwa mfumo wa umeme kwenye ubongo.