Mwandani wa huduma ya usafiri wa mabasi ya UDA jijini Dar es Salaam kwa ufupi

Mwandani wa huduma ya usafiri wa mabasi ya UDA jijini Dar es Salaam kwa ufupi

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
242
Reaction score
1,141
1000084558.jpg

Toka kuanzishwa kwake mwaka 1947 kampuni ya usafiri wa mabasi jijini Dar es Salaam Motors Transport (DMT) chini ya udhibiti wa British Holding Cooperation United, iliendesha shughuli zake kama katika nchi zilizoendelea. Yaani mabasi yalikuwa yanakwenda sio kiholela bali kwa ratiba na kitabu chake ndicho hicho hapo juu.

Lakini mara baada ya sekta nzima za uchumi kuwa mikononi mwa umma, mwaka 1970 mchakato huo ulitumika kutaifishwa kwa DMT, iliyokuwa kampuni binafsi ya Uingereza iliyokuwa ikifanya kazi ya kusafirishs abiria wa jiji peke yake.

Shirika la UDA lililoanzishwa tAprili 4, 1974 na kurithi huduma kutoka DMT hadi Mei 1974 wakati Usafiri Dar es Salaam (UDA) ilipewa jukumu la kutoa huduma za abiria wa jiji la Dar, huku Kampuni ya Mabasi Tanzania (KAMATA) ikawa na jukumu la kutoa huduma abiria wa mikoani.

Bahati mbaya utendaji wa UDA ukaanza kuzorota hasa baada ya kupungua idadi ya mabasi kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kufanya kazi kwa mazoea na kukosa ruzuku waliyohitaji kununua mabadi na spea. Yaani Kinikia linaonesha upungufu ulikuwa kutoka mabasi 257 mwaka 1975 hadi kufikia 12 tu mwaka 1998!

UDA imekuwa ikijikongoja kwa zaidi ya miaka 60, huku sekta binafsi ikikomba mboga yote kupitia daladala zao zilizoanza kama chai Maharge hadi mabasi makubwa.

Hata hivyo serikali ikaibuka na kujiongeza. Kwanza ikafungua UDA Rapid Transit Ltd (UDA-RT), ambalo ni tawi la uwekezaji la UDA ili kuendesha Mradi huo wa DART, huku ikijenga barabara mahususi kwa mabasi hayo, na kuleta faraja kwamba mambo yatakuwa mswano muda si mrefu ujao.

Issa Michuzi
 
Back
Top Bottom