Mwandiko mzuri, kichwani hamna kitu. Hii ndio elimu ya TZ

Halafu tunashangaa kwa nini wamefeli kwa kishindo!!
Je hiyo tume imeundwa kuchunguza nini??!

Neno tume limepoteza kabisa maana katika hii nchi yetu. Mi nasubiri tu kusikia tume imeundwa na huyu rais kuchunguza kwa nini kila jioni maji yanatoka bahari kuu na kujipigiza karibu na ikulu. Eti tume!!! neno halina maana kabisa siku hizi...
 
Hahahaaaaaa!!!!!!!!!!!!! huyu ni kiboko nadhani alikuwa anavuta muda ufike ili ajitokee
 
Tatizo ni lugha. Km angelijibu kwa Kiswahili, angeliandika kitu chenye kuleta maana hata km jibu lisingelikuwa sahihi.
 
duh....umenichekesha mkuu!!! na huyu alikua anatarajia kwenda a-level tena pcb mhhh!!! hapa kazi ipo....ivi ule mtihani wa fom2 upo...nadhani ungepunguza haya matatizo...
 
Mbona hii kali sana, bora asingejibu kabisa lijulikane moja kuliko kumchosha msaishaji katika kutafuta ilipo point.
 
dah!! YAANI HUYU KILA KANENO KA KIINGEREZA KANAKOINGIA KICHWANI ANAKAANDIKA KWENYE KARATASI ha ha haaaaa....kweli si mchezo, afadhali hata ya waziri wake Mulugo wa "Tanzania got its independence on one nineteen sixty one".
 
Bado tupo kwenye msiba wa ndugu zetu form four hivyo tuungane wote kwa kusema "NECTA IMETOA NECTA IMETWAA, FORM FIVE WALIIPENDA LAKINI KITAA KIMEWAPENDA ZAIDI."
 
sijui kama watoto hawa wanajua 1+1 ni ngapi?
ukimuuliza anaweza akajibu haiwezekani
Haya ni matokeo ya shule za msingi zinazopasisha watoto wasioujua kusoma na kuandika na kuhesabu/
 
....this is a joke bujibuji, right?

A joke??? How can it be a joke while you see it to be a scanned script wrote by a candidate? Habari ndiyo hiyo mkuu. Next time you see here a teacher being insulted spare a second or two to think what we poor souls are going through!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…