Mwandishi aliyeko kizuizini Uganda afikishwa Mahakamani

Mwandishi aliyeko kizuizini Uganda afikishwa Mahakamani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwandishi wa Uganda anayetuhumiwa kutuma taarifa za kashfa kuhusu rais na mtoto wake wa kiume kwenye mtandao wa Twitter amefunguliwa mashtaka mahakamani, wiki kadhaa baada ya kukamatwa.

Kakwenza Rukirabashaija alishtakiwa kwa makosa mawili ya mawasiliano ya kukera na amepelekwa gerezani hadi Januari 21, atakapofikishwa tena mahakamani.

Wakili wake Eron Kiiza alisema mwandishi huyo alikuwa akichechemea, na aliiambia mahakama kuwa afya yake inadhoofika. Wakili huyo hapo awali alisema kuwa mteja wake aliteswa aliipokuwa kizuizini.

Bw Rukirabashaija alikamatwa mwezi Disemba na wiki iliyopita, mahakama iliamuru aachiliwe bila masharti lakini mamlaka haikuzingatia agizo hilo.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom