Fadhili Paulo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2011
- 3,211
- 993
[h=5]Mwandishi atoa ushahidi kesi ya madaktari
Na Waandishi wetu
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mtanzania Benjamin Msese ametoa ushahidi mahakamani na kudai kwamba Juni 27, mwaka jana, Dk. Namala Mkopi, alitoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari na kulaani kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka.
Alidai kuwa katika tamko hilo, Dk. Namala alisema kitendo hicho ni cha kinyama na hakikubaliki pia Serikali inaweza kuhusika kwani ilikataa kutoa gari la Muhimbili na wao kutumia la Kampuni binafsi kumpeleka Dk. Ulimboka hospitalini.
Shahidi huyo alitoa ushahidi wake huo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi inayomkabili Rais wa Chama cha Madaktari nchini (MAT), Dk. Namala Mkopi.
Ushahidi huo ulitolewa mbele ya Hakimu Hellen Liwa na upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili Kashinyi Mtalemwa huku upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Kikondo Maulid.
Shahidi huyo aliiambia Mahakama kuwa siku ya mgomo wa madaktari Juni 27, mwaka jana akiwa katika ufuatiliaji wa mgomo wa madaktari uliokuwa ukiendelea nchini alifika Muhimbili akitokea Amana Hospitali na kupata taarifa za kujeruhiwa kwa Dk. Stephen Ulimboka.
Aidha, alisema baada ya kufika huko alimkuta Msaidizi wa Dk. Ulimboka, Deogratius Michael ambaye aliwaeleza yaliyojiri na kuwaambia MAT ingetoa tamko siku hiyo.
Masese alidai kuwa ahadi hiyo ilitimia saa 8 mchana, tamko lilipotolewa mbele yao na Dk. Namala ambaye alisema MAT inalaani kitendo cha kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka.
Aliendelea kudai kuwa Mkopi alisema kwasababu ya kutekwa kwa Dk. Ulimboka wao kama madaktari wataendelea na mgomo pia kuwasihi wenzake waongeze nguvu kumtibu Dk. Ulimboka.
Shahidi huyo alidai mahakamani hapo kuwa habari hizo ziliandikwa Juni 28, mwaka jana katika Gazeti la Mtanzania toleo Na. 6099 na lilisomeka kwa kichwa cha Habari kilichosema NI UNYAMA na Mahakama ilipokea Gazeti hilo kama kielelezo cha pili.
Hakimu Liwa aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 12, mwaka huu na kuuambia upande wa Jamhuri kuita mashahidi wengine.
Awali, Dk. Namala alifikishwa mahakamani hapo Septemba mwaka jana akiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kukaidi amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ya kuwataka madaktari kusitisha mgomo na shtaka la pili likiwa la kushawishi madaktari wagome.
CHANZO: NIPASHE[/h]