Mwandishi Mkuu Gazeti la Mwananchi ashauri Serikali kubadili msimamo Uraia pacha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Mwandishi Mkuu MCL ashauri Serikali kubadili msimamo uraia pacha.jpg
Dar es Salaam. Mwandishi wa Habari Mkuu wa Gazeti la Mwananchi, Elias Msuya ameshauri Serikali kutazama upya msimamo wake kuhusu zuio la uraia pacha, akisema uraia pacha utasaidia kufungua milango kwa Watanzania na fursa za Taifa kunufaika kiuchumi.

Msuya ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Mei 31, 2023 wakati wa mjadala wa Twitter Space ya Mwananchi Communications Limited (MCL) yenye mada ‘una maoni gani kuhusu suala la uraia pacha Tanzania.’

Mjadala huo unafanyika ikiwa ni siku moja imepita tangu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Dk Stergomena Tax kuelezea Bunge jana Jumanne, Mei 30, 2023 Serikali inakamilisha mchakato wa kutoa hadhi maalum kwa Diaspora.

Jumatatu ya Mei 29, 2023 Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Mhandisi Hamad Masauni aliliambia Bunge hadi kufikia Mei 2023, Watanzania 66 waliukana uraia wa Tanzania na kupewa uraia wa Mataifa mengine.

Akichokoza mada kwenye mjadala huo, Msuya amesema, “suala la uraia pacha halina muafaka duniani, lakini nimefutilia nikagundua kwamba mataifa mengi yanaunga uraia pacha kuliko yanayopinga uraia pacha duniani, hatua hiyo inamaanisha, mataifa mengi yameanza kuona umuhimu wa uraia pacha.”

“Kuna hofu watu wakiwa na uraia pacha kupora rasilimali za Tanzania kupeleka nje ya nchi. Kuna watu wanamilikishwa ardhi ni wageni lakini hawana uraia pacha, sasa hoja ya kupora mbona inaonekana bila hata kuwepo uraia pacha?

“Uraia pacha utatoa fursa, wananchi wakafute maisha na kuleta uwekezaji na fursa za maisha, matokeo yake ni kwamba nchi itaenndelea.”

“Watanzania wanapokwenda kuishi nje ya nchi wanakuwa huru kuleta utajiri wanaoupata na kama nchi tunajikuta tunaongeza mapato ambayo yanapatikana kupitia fedha zinazoletwa na watu waliokwenda nchi nyingine.”

Chanzo: Mwananchi

Pia soma: Serikali yatoa msimamo kuhusu uraia pacha
 
Elimu iendelee kutolewa kwa hawa WATAWALA wetu ,ipo SIKU wataelewa tu ,ni kama issue ya KATIBA MPYA...walishupaza shingo,mwisho wa SIKU wamekubali..
 
Hatukubali Uhuni wa uraia pacha.
Hauna taarifa sahihi tu. Nchi yako hailiwi na diaspora. Hawa ni Watanzania wenzio waliokwenda kutafuta maisha kama kijana ye yote anavyoweza kwenda akipata nafasi badala ya kukaa mtaani tu bila ajira.

Na wanatuma nyumbani ma trillioni ya shilingi kila mwaka japo yanaishia kuliwa na wazalendo. Kwa wajanja huko Rwanda diaspora wanatambuliwa kama mkoa kamili unaojitegemea.

Nchi yako inaliwa na wazalendo walioko hapahapa wenye kuvaa ma-scarf ya bendera ya taifa kila waendako; na kugonga meza mjengoni kuunga mkono kila kitu. Uhuni uko huko na hasira zako zielekeze huko!
 
Hivi ki ukweli ukiwa mtanzania kwa kuwa tu una pass ya nje nini kinakwama kufanyika nyumbani maana mi sielewi .
 
Dhamira yenu sio nzuri kwa Taifa Tanzania.

Kule Kenya kwenye Makao yenu makuu ndio mnapaswa kupeleka huu utopolo sio Tanzania.
Unaweza ukatanabaisha hapa hiyo dhamira mbaya iliyo nyuma ya wataka uraia pacha kwanini tunashindwa kufikiria vizuri karne ya 21 bado tunakomaa na mawazo ya kijima mbona pesa za hao diaspora tunazitaka nafikiri hatuna budi kubadili mtazamo wetu juu ya hili suala na kuacha hofu ya isiyo na mashiko
 
Hauna taarifa sahihi tu. Nchi yako hailiwi na diaspora. Hawa ni Watanzania wenzio waliokwenda kutafuta maisha kama kijana ye yote anavyoweza kwenda akipata nafasi badala ya kukaa mtaani tu bila ajira. Na wanatuma nyumbani ma trillioni ya shilingi kila mwaka japo yanaishia kuliwa na wazalendo. Kwa wajanja huko Rwanda diaspora wanatambuliwa kama mkoa kamili unaojitegemea.

Nchi yako inaliwa na wazalendo walioko hapahapa wenye kuvaa ma-scarf ya bendera ya taifa kila waendako; na kugonga meza mjengoni kuunga mkono kila kitu. Uhuni uko huko na hasira zako zielekeze huko!
Sehemu kubwa ya wenye access ya kuwa diaspora nchi hii ndiyo hao hao na watoto wao wanatafuna nchi huku. Sehemu kubwa ya wabadhirifu hao ndiyo wanapigania uraia pacha ili wao na wana wao watunyonge vizuri. Kama tunataka uraia pacha basi uwe accessible kwa wote. Tuanze na suala la passport na Visa. Hata mama muuza vitumbua na Chinga akitaka passport na visa aipate kiurahisi kama mtoto wa tajiri au mwanasiasa anavyoipata. Ikiwezekana huyu asaidiwe zaidi.

Kinyume na hapo uraia pacha ni kuwaongezea wabadhirifu uwanja wa kutupiga.
 
Uraia picha No no....no
tutatengeneza tatizo kubwa la kiusalama endapo tutaruhusu suala la uraia pacha, lisiwepo na kamwe lisikubaliwe
Kama unaweza kuweka hapa hilo tatizo la kiusalama litakalo tokana na Watanzania kupewa uraia pacha tafadhari tanabaisha hapa maana kuna hofu isiyo na mashiko inaenezwa hasa na wanasiasa
 
Hata mataifa makubwa kama Ujerumani walikataa suala la Uraia pacha sembuse sisi Watanzania!!

Hatutaki uraia Pacha katiaka nchi yetu.
 
View attachment 2642027
Dar es Salaam. Mwandishi wa Habari Mkuu wa Gazeti la Mwananchi, Elias Msuya ameshauri Serikali kutazama upya msimamo wake kuhusu zuio la uraia pacha, akisema uraia pacha utasaidia kufungua milango kwa Watanzania na fursa za Taifa kunufaika kiuchumi.

Msuya ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Mei 31, 2023 wakati wa mjadala wa Twitter Space ya Mwananchi Communications Limited (MCL) yenye mada ‘una maoni gani kuhusu suala la uraia pacha Tanzania.’

Mjadala huo unafanyika ikiwa ni siku moja imepita tangu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Dk Stergomena Tax kuelezea Bunge jana Jumanne, Mei 30, 2023 Serikali inakamilisha mchakato wa kutoa hadhi maalum kwa Diaspora.

Jumatatu ya Mei 29, 2023 Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Mhandisi Hamad Masauni aliliambia Bunge hadi kufikia Mei 2023, Watanzania 66 waliukana uraia wa Tanzania na kupewa uraia wa Mataifa mengine.

Akichokoza mada kwenye mjadala huo, Msuya amesema, “suala la uraia pacha halina muafaka duniani, lakini nimefutilia nikagundua kwamba mataifa mengi yanaunga uraia pacha kuliko yanayopinga uraia pacha duniani, hatua hiyo inamaanisha, mataifa mengi yameanza kuona umuhimu wa uraia pacha.”

“Kuna hofu watu wakiwa na uraia pacha kupora rasilimali za Tanzania kupeleka nje ya nchi. Kuna watu wanamilikishwa ardhi ni wageni lakini hawana uraia pacha, sasa hoja ya kupora mbona inaonekana bila hata kuwepo uraia pacha?

“Uraia pacha utatoa fursa, wananchi wakafute maisha na kuleta uwekezaji na fursa za maisha, matokeo yake ni kwamba nchi itaenndelea.”

“Watanzania wanapokwenda kuishi nje ya nchi wanakuwa huru kuleta utajiri wanaoupata na kama nchi tunajikuta tunaongeza mapato ambayo yanapatikana kupitia fedha zinazoletwa na watu waliokwenda nchi nyingine.”

Chanzo: Mwananchi

Pia soma: Serikali yatoa msimamo kuhusu uraia pacha
na kwa nn mnakana uraia wenu.nyinyi si wazalendo na swala la uraia pacha lina hasara zaidi kuliko faida.
 
Hata mataifa makubwa kama Ujerumani walikataa suala la Uraia pacha sembuse sisi Watanzania!!

Hatutaki uraia Pacha katiaka nchi yetu.
Uko na ushahidi wa unayoyasema kwahiyo kama unachosema ni sahihi na sisi tufate mkumbo mbona zipo nchi nyingi tu zinakubali uraia pacha
 
Back
Top Bottom