Mwandishi Munga Tehenan: YUPO WAPI?

Phillemon Mikael

Platinum Member
Joined
Nov 5, 2006
Posts
10,557
Reaction score
8,673
Wadau naomba kujuwa alipo mwandishi maarufu wa makala, na one time mhariri na mmiliki wa gazeti la JITAMBUE.

Ameandika vitabu vingi vya lugha na hadithi, na kuna wakati alikuwa na TALK SHOW pale TBC1 Wakati ikiwa TVT. Pia amewahi kuwa Majira Publishers, nadhani mhariri wa vitabu among other things...

MHARIRI, MUNGA TEHENAN!
 
Marehemu Munga pia alikuwa akiandika makala za Saikolojia katika magazeti mbalimbali ambazo kwa kiasi kikiubwa zilitusaidia Watanzania na kutuongoza katika mambo mbalimbali yahusuyo maisha ya kila siku.

Binafsi ni mpenzi mkubwa wa makala na vitabu vya Hayati Munga Tehanan
 
Heshima mbele mkuu!..MUNGA TEHANAN kwa sasa ni marehemu mkuuu,alifariki tarehe 5/8/2008 katika hospitali ya Hindu Mandal ambako alilazwa kwa muda mfupi akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo

Sure.
Huyu bwana ni kweli alifariki mwezi wa nane.
Tutamkumbuka kwa makala zake za kisaikolojia.
Mungu amlaze mahala pema
 
Sure.
Huyu bwana ni kweli alifariki mwezi wa nane.
Tutamkumbuka kwa makala zake za kisaikolojia.
Mungu amlaze mahala pema

Sory mkuu nilipitiwa kidogo,alifariki tarehe 5 Mei 2008,nimesahihisaha hapo juu
 
..du sikuamini nilisikia kwa mtu kuwa amefariki .....lakini kwa mchango mkubwa wa MUNGA kwenye uandishi sijui hapa jamii tulipitiwa vipi kumpa heshima stahili...alafu nikashangaa sana hata sujaona makala za waandishi na wahariri wenzake kwenye televisheni na magazeti kumuenzi........nadhani hata hakuna tv wala redio iliyotangaza kifo chake wakiwemo TBC[TVT ] ambako alikuwa akiandaa talk show nzuri sana kwenye kile kipindi kigumu....

KWA KWELI NINAYO HESHIMA KUBWA SANA KWA MUNGA TEHENAN ,,,,..MWANDISHI MAHIRI...

NAOMBA HAPA JF WANAOMJUWA ZAIDI TUTUMIE FURSA HII KUTIZAMA LEAGACY YAKE!!!!

RIP...
 
RIP MUNGA...

Nimesoma sana makala zake zilizojaa MAFUNDISHO, ni vyema tukawa na utaratibu wa kuwaenzi watu muhimu kama hawa, tusisubiri serikali maana Mkuchika ndio huyo anaziba midomo waandishi wa habari.
 
Heshima mbele mkuu!..MUNGA TEHANAN kwa sasa ni marehemu mkuuu,alifariki tarehe 5/5/2008 katika hospitali ya Hindu Mandal ambako alilazwa kwa muda mfupi akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo
Alilazwa katika nyumba yake ya milele pale katika makaburi ya Kisutu, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Munga Tehenani mahala pema peponi, Amen.
 
Alilazwa katika nyumba yake ya milele pale katika makaburi ya Kisutu, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Munga Tehenani mahala pema peponi, Amen.

Ni kweli alitutoka kimwili kama mwenyewe alivyopendelea kusema.

Mojawapo ya makala zake ambayo ilichukuliwa kama ilikuwa ikitabiri kifo chake ni hii ambayo nitaiweka hapa chini.

Na ni kweli hayao yote aliyo yaandika yalitokea kwenye msiba wake, nadhani waliohudhuria watakumbuka zaidi.

 
RIP Munga, nazikumbuka sana makala zako kwenye gaziti la 'Jitambue'.

Munga ni mmoja ya watu ambao wananifanya nitamani kuwapo kwa teknologia ambayo binaadamu tunaweza ku'copy' kumbukumbu kutoka kwa mtu mmoja na kuhamishia kwa mtu mwingine au tu kuzihifadhi (I mean to copy intelligence from a person before he dies so that we can later on paste into one or more other living persons or access it for other uses).
 
Duu! life is too short! yule jamaa nilikuwa napenda kipindi chake kile cha vijana TBC1, hata sikujua kama alisha tutangulia.

pumzika kwa amani kaka!
 
Munga Tehenan, nilianza kumsoma kwenye Jitambue, na kweli nikajitambua, nikaja kumsikiliza Radio Tumaini na Baadaye TVT, kwa kweli habari ya kifo chake imenisikitisha sana sana.

RIP Munga
 
Kwa hakika, inaumiza sana kwamba alipofariki hakuna hata makala moja iliyoandikwa juu yake na waandishi wenzake. kama ipo, nipo tayari kukosolewa. Ametutoka kimya kimya mno kwa mtu aliyekuwa na jina kubwa katika sanaa ya habari kama yeye. Mdau uliyeleta makala ya Munga umenishitua sana kwamba hata kwenye msiba wake kulitokea mambo kama aliyoandika. Inasikitisha.
 
Ndugu zanguni, nimeshtushwa sana na habari hii,
Kumbe ndugu yetu Munga Tehenan alishatangulia mbele ya haki?

Bwana alitoa, na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen.
 
Pumzika Kwa Amani MUNGA TEHENAN.
alikuwa mwandishi makini na mwenye fasihi nyingi,binafsi nilipenda sana magazeti yake yote mawili.
kuna baadhi tu yamakala zake ambazo unaweza zipata kwenye web site yake
www.tkmedia.co.tz
 
i never knew munga,and dont even remember reading any of his articles,but from what i have been reading in the forum,it seems society has lost a titan.may his soul rest in peace.AMEN
 
Nasikitika baada ya Munga gazeti la Jitambue limekufa
 
Jitambue lilikuwa gazeti mahiri sana ambalo bwana Munga alikuwa Mhariri wake. Gazeti hilo lilikuwa likiandika makala kem kem zilizohusu saikolojia.Mambo mengi yalijadiliwa katika Gazeti la Jitambue kama vile ndoa, mapenzi, mafanikio,elimu,afya,ubongo na mengineyo ambayo kwasasa siyakumbuki. Mimi nilikuwa msomaji wa Gazeti hilo na mwaka 2006 na 2007 nilifanikiwa kununua nakutunza nakala zote za Gazeti hilo . Kwasasa naona Jitambue limekufa.Ila naona website yao bado ipo, ikiwa na makala chache.

Nakiri kwamba tumepoteza mwandishi mahiri sana. Lakini katuachia urithi wafikra na elemu yake katika Saikolojia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…