Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Kwanza nianze kwa kusema kuwa ufreemason unaozungumzwa hapa si ule wa kwenye nguzo za umeme. Ni ule wa watu wenye fikra huru wanaokusanyika pamoja ili kuboresha maisha ya binadamu.
Kwa nini nauliza iwapo Shaaban Robert alikuwa ni freemason? Kuna huu ushahidi.
1. Nilikuwa nasoma kitabu cha Shaaban bin Robert kiitwacho Siku ya Watenzi wote. Katika kitabu hiki Mwandishi anazungumza kuhusu jumuia iitwayo Jumuia ya Adili. Jumuia hiyo ni kama jumuia ya kidini lakini haina dini. Watu wa dini zote wanakaribishwa. Kila jumamosi ibada ya dini zote hufanyika katika jumuia hiyo. Kazi kubwa ya jumuia hii ni kusaidia wenye uhitaji. Watu hupeleka sadaka zao kwenye jumuia hiyo bila ya maonyesho.
Jumuia hiyo inafanana sana na ufreemason ambao watu wa dini zote hujiunga na kazi yake kubwa kuboresha maisha ya mwanadamu. Kitabu hicho unaweza kukisoma bure ndani ya app ya Maktaba Sauti, ipo playstore.
2. Wote tunamfahamu Marehemu Sir Andy Chande aliyekuwa kiongozi wa freemasons Tanzania. Kwenye kitabu cha maisha yake kaandika jinsi ambavyo alikusanya watu ili waanzishe shule. Na shule hiyo wakaiitaje? Shaaban Robert! Kwa nini shule iliyoanzishwa na freemasons iitwe jina la Shaaban Robert? Je alikuwa ni mwenzao?