Mwandishi Oscar Oscar achukua fomu kugombea nafasi ya Urais TFF

Mkuu GENTAMYCINE tumemuita hivyo kulingana na anavyojiita akihojiwa kwenye Social Media na vile vile anavyojitambulisha hasa kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Lakini umetupa somo bomba kuwa unajua Kinagaubaga jinsi alivyokuwa hapo awali na mpaka hivi wa leo, asante sana.

Ni Mchambuzi ambaye yupo vizuri na huwa namfuatilia kwenye michezo na naungana nawe kuwa hana mpinzani, ukiachilia mbali ule Uchale wake anaofanya kwenye ukurasa wake wa Instagram 'Kipa Katoka'.
 
Hapa Tanzania kuna mtu ambaye siyo shabiki wa simba au Yanga?
 
Hakuna.

Yaani ni kama jinsia tu, ni either uwe mwanaume au mwanamke.
Mimi mwenyewe ni mwanasimba lialia na siwezi kulificha hilo. Hata akina mama lazima utakuta wamegawanyika hivyo.

Karia kajitahidi sana kuendesha soka letu kwa weledi na ule wizi wizi pale TFF umepungua.

Chini ya Karia ligi yetu imeboreka sana ndiyo maana tunapata na udhamini mkubwa wa haki za matangazo tu wameweka program ya kuboresha viwanja,kuna ligi ya wanawake na mdhamini yupo, ligi ya under 17, ligi ya under 20.timu yetu ya taifa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 chini ya uongozi wa Karia imecheza AFCON ndani ya muda huo huo Simba Katinga robo fainali CAF mara mbili, Namungo kacheza hatua ya makundi.

Baada ya Tenga Karia ndiyo kiongozi sahihi wa TFF.
 
Earphone huku tunaongea hicho ni kiburi na inamaanisha hauko vizuri katika kusikiliza.
Yeye Oscar na Kitenge wanapenda mno kuwa na Earphone muda wote sijui kwanini...!
 
Ni kama mtu kusema Mimi sina Chama, lakini kwenye mijadala ya siasa hakosekani.
Hapa Tanzania mtu lazima atakuwa simba au Yanga unless awe hajawahi kuzifahamu hizo timu.

Simba na Yanga ni maisha ya watanzania watoto wanazaliwa wote simba na Yanga
 

Ila kuongoza mpira kwa nchi ambazo siasa zinaathiri utendaji ni changamoto sana.

Binafsi Tenga ningetamani aendelee uongozi kwa vipindi vingi zaidi, maana jamaa alipiga kazi sana.
 
Ndiyo Mchambuzi pekee wa Michezo nchini Tanzania ambaye ( japo ni Simba SC hasa ) ila akiwa Kazini EFM ( anachambua ) huwezi kujua kama ni Simba au Yanga tena mara nyingi kukifanyika ' Upuuzi ' Simba SC Kwetu ndiyo huwa ' anatuponda ' kweli kweli na 75% ya ' Uchambuzi ' wake huwa unafanyiwa Kazi na Simba SC, Yanga SC na hata huko TFF Kwenyewe.

Binafsi namkubali na ana 'IQ'Kubwa pia.
 
Punguza chuki mtoto wa kiume,pesa zake na ww tafuta zako
 
oscar oscar wa instagram na huyu aliyechukua fomu ni watu wawili tofauti ata ukimsikilza akiwa redioni jamaa ana madini kichwani ya mpira
 
Yeye Oscar na Kitenge wanapenda mno kuwa na Earphone muda wote sijui kwanini...!
Oscar Oscar ndiye amemuiga huo Mtindo Maulid Kitenge na siyo Siri Mtu aliyembadilisha na Kumtambulisha katika dunia hii ya Kisasa Oscar Oscar ni Maulid Kitenge na Vitu vingi ( hasa vya Kimaisha ) avifanyavyo Oscar Oscar anamuiga Maulid Kitenge ambaye huko nyuma walikuwa ni ' Washkaji ' wakubwa sana ila kwa sasa Urafiki wao uko Rehani ( si ule tena ) kwani kuna Mgodi Mmoja wa ' Kibaiolojia ' wanauchimba wote na huo Mgodi umetokea ' Kumkubali ' zaidi Mchimbaji Oscar Oscar.
 

We jamaa bana dah!

Sijui unatoaga wapi hizi habari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…