Mwandishi wa habari wa Ayo TV, Eugene Peter amepotea na hajulikani alipo. Familia yake inamtafuta

Mwandishi wa habari wa Ayo TV, Eugene Peter amepotea na hajulikani alipo. Familia yake inamtafuta

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mwandishi wa Habari Eugen Peter anatafutwa na Familia yake pamoja na Ofisi yake ya Ayo TV Dar es salaam baada ya kutoweka bila kujulikana alipo leo ikiwa ni siku ya tisa.

Mara ya mwisho Eugene alionekana mazingira ya nyumbani kwake Jumapili December 29,2024 majira ya saa mbili usiku.

Familia akiwemo Baba yake Mzazi na Watu wa karibu wamethibitisha kutokuwa na mawasiliano naye tangu wakati huo ambapo Dar es saalam hajaonekana na kwao Arusha na Moshi hajafika huku simu zake zikiwa hazipatikani.

Baada ya jitihada kubwa za kumtafuta maeneo mbalimbali na kutoa taarifa ya kupotea kwake Polisi, AyoTV na Familia kwa pamoja tunaombat mtu mwenye taarifa kumuhusu apige simu namba 0748400047 au aripoti kituo cha Polisi kilicho karibu nae

EP.png

Source: Millard Ayo

Kwa update ingia hapa: Mwandishi wa habari wa Ayo TV, Eugene Peter apatikana MOI, alipata ajali ya Bodaboda
 
Jamani,jana yule wa Tv3 amepatikana kwa shangazi yake...... yaani siku hizi mtu asipoonekana tu kwenye mitandao ya Simu, tayari kapotea........kuna kitu kimejengwa kwenye jamii yetu hakiko sawa
 
Zamani kesi nyingi za kupotea watu, ziliwahusu watoto na wale ndugu zetu wenye changamoto ya afya ya akili! Ila cha kushangaza siku hizi kesi za aina ile ile, zinawahusu watu wazima na wenye akili zao timamu! Nadhani kuna tatizo mahali.
 
Kupotea ,Kutoweka
Siku ya tisa bado hakuna taarifa za mtu aliepotea,dah
 
Zamani kesi nyingi za kupotea watu, ziliwahusu watoto na wale ndugu zetu wenye changamoto ya afya ya akili! Ila cha kushangaza siku hizi kesi za aina ile ile, zinawahusu watu wazima na wenye akili zao timamu! Nadhani kuna tatizo mahali.
Hakika mkuu kuna tatizo mahali
 
Alafu Millard Kaja kutoa taarifa juzi, siku moja kabla ya kupatikana!?!

Mtangazaji wake alinyangwanya vifaa na makonda akala buyu, hii nayo siku zote alikaushia dah.

RIP Ulomi
 
Back
Top Bottom