Mwandishi wa habari wa Ayo TV, Eugene Peter apatikana MOI, alipata ajali ya Bodaboda

Mwandishi wa habari wa Ayo TV, Eugene Peter apatikana MOI, alipata ajali ya Bodaboda

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mwandishi wa Habari Eugen Peter ambaye leo asubuhi kupitia kurasa za Millard Ayo alitangazwa kutokujulikana aliko, amepatikana mchana huu akiwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dar es salaam.

Soma pia: Mwandishi wa habari wa Ayo TV, Eugene Peter amepotea na hajulikani alipo. Familia yake inamtafuta

Kwa mujibu wa MOI, Eugen alifikishwa Hospitali hapo December 31,2024 akitokea Hospitali ya Mwananyamala akiwa amepoteza fahamu na akiwa na majeraha mikononi na kichwani yanayotajwa kuwa yamesababishwa na ajali ya pikipiki ambapo alilazwa kama Mgonjwa asiyejulikana utambulisho wake ( unknown ).

Eugen ambaye wakati wa kutoweka kwake alikuwa amechukua likizo ya kazi mwishoni mwa mwezi December, hakwenda nyumbani kwao Arusha kama ilivyotarajiwa wala hakuonekana nyumbani kwake Ubungo na simu zake hazikuwa zikipatikana ndipo Ndugu, Jamaa na Marafiki wakishirikiana na Ofisi yake (AyoTV) walipoanza kumtafuta katika maeneo mbalimbali.

Pia soma: Watu wanaopotea/kutekwa karibuni kupatikana kwa ndugu/jamaa kuna jambo linatengenezwa, there are no coincidences!

AyoTV inawashukuru wote walioshiriki katika jitihada za kumtafuta na wale wote waliofanikisha kupatikana kwake ikiwemo Taasisi ya MOI.
Screenshot 2025-01-06 140613.png
 
Back
Top Bottom