Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Tunatoa pole kwa familia
Moshi. Mwandishi wa habari wa redio Moshi FM, Deogratius Kessy (26) amefariki dunia katika ajali baada ya gari alilokuwa amepanda kuacha njia na kugonga bajaji.
Kessy alikuwa akitangaza kipindi cha burudani cha The base show katika redio hiyo.
Kifo cha mwandishi huyo kimetokea ikiwa zimepita siku 35 tangu mwandishi mwingine wa habari wa redio Kili FM mjini Moshi, Benedick Kuzwa kufariki dunia katika ajali.
Akizungumza leo Jumamosi Desemba 12, 2020 kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Emmanuel Lukula amesema ajali hiyo imetokea jana saa 2 usiku katika barabara ya Getifonga eneo la kona ya kibao cha kuelekea Kahe.
Amesema gari aina ya Noah lililokuwa limepakia watu zaidi ya wawili likitokea Newland kwenda mjini Moshi ilipofika katika kona hiyo liligonga bajaji na kuwajeruhi watu watatu na mwandishi huyo kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitali ya rufaa Mkoa wa Kilimanjaro.
“Kwenye ile Noah watu wawili walipata zaidi majeraha na waliwahishwa hospitali ila mmoja ndio amefariki. Kwenye ile bajaji mama mmoja alivunjika miguu yote miwili na majeruhi wote wanaendelea na matibabu,” amesema.
Akizungumza na Mwananchi Digital meneja vipindi wa redio hiyo, Rodrick Makundi amesema, “tumepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa hakika tutamkumbuka Deogratius kwa mambo mengi mazuri kwani alikua mchapakazi mzuri. Alikuwa anatoa ushauri pale unapohitajika pia tulijifunza mambo mengi mazuri kutoka kwake kutokana na ubunifu wake kwenye vipindi alivyokua akifanya.”