Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Viongozi Afrika Mashariki wameingiwa na pepo gani?
Kutoka nchini Kenya mwandishi anayejulikana kwa jina la Bruce John ameripotiwa kuteswa na kulawitiwa mara baada ya kufichua uovu wa Gavana wa Mombasa.
Bruce kupitia mfululizo wa video zilizowekwa kwenye mtandao wa Tiktok alidokeza kuwa alitekwa na watu waliojitambulisha kama maafisa wa Jeshi la Polisi la Kenya ambao walimchukua na kumpeleka kwenye eneo lisilojulikana.
Baada ya kumfikisha kwenye eneo hilo vijana hao walimtesa na kisha baadaye kumlawiti kwa zamu na kumrekodi.
Bruce aliongeza kuwa mara baada ya kumrekodi, vijana hao walimtishia kuwa iwapo angeenda kuwashtaki basi wangeachia video hiyo na kuongeza kuwa baada ya muda aliwasikia watekaji hao wakiongea na Gavana wa Mombasa ambaye pia aliwatumia kiasi cha 10,000 za Kenya.
Bruce aliendelea kusimulia kwa kusema kuwa baada ya vijana hao kumfanyia unyama huo walimpiga kiasi cha yeye kuzimia kisa kumtelekeza kwenye jumba bovu.
Baada ya kuzinduka, Bruce alianza kutafuta njia ya kwenda nyumbani ambapo baada ya kufika alianza utaratibu wa kupata matibabu.
Alidokeza kuwa alipopelekwa hospitali, madaktari wa kwenye hospitali ya kwanza hawakumpa matibabu yanayoeleweka kwa sababu ya hofu kuwa kesi hiyo ina uhusiano na Gavana wa Mombasa na ndipo alipopelekwa kwenye hospitali ya pili ambapo ndipo anaendelea na matibabu hadi sasa.
Mara baada ya stori ya Bruce kufika kwenye mitandao ya kijamii, wanaharakati mbalimbali wa haki za binadamu wamejitokeza kutetea haki za mwanahabri huyo kwa kuiomba serikali ya Kenya kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini wote waliofanya unyama huo
Soma Pia: Mwandishi wa Media Max Limited Catherine Wanjeri apigwa risasi Nakuru, akifuatilia maandamano ya Wananchi kupinga serikali