On Duty
JF-Expert Member
- Aug 21, 2020
- 566
- 1,083
Ni matumaini yangu kwamba ewe msomaji ubuheri Wa afya.
Leo nimekuja na makala fupi ambayo itatupa mwongozo na kutufanya tujikwamue Kutoka gizani(kwenye kiza) na kutufanya tuifikie nuru. Makala hii imejikita zaidi katika elimu na maendeleo ya mtanzania na Mwafrika kwa ujumla.
Unaelewa nini kuhusu Elimu?
Elimu ni maarifa alishwayo(apewayo) mtu kuhusu kitu fulani. Kama wewe unapewa kitu ambacho haukuwa nacho au haukuwa ukikijua basi hapo tunasema unapewa elimu kuhusu hicho kitu. Siku zote yule anayekupa Elimu huwa na malengo ya kwamba wewe uweze kupata ufahamu kuhusu Elimu hiyo anayokupa.
Mwanga ni nuru ambayo inakuwezesha kuona kitu fulani. Na giza ni ukosefu wa mwanga. Najua msomaji utaanza kujiuliza kwanini ni kiza badala ya giza?, usipate taabu kuhusu hilo, kiza ni giza nene. Hivyobasi, kiza na giza ni kitu kilekile tu.
Jinsi gani tupo gizani kielimu?
Katika jamii yetu(zetu) hapa nchini na Afrika kwa ujumla kumekuwa na utamaduni wa kuaminishana kwamba, mtu usome uje upate kazi nzuri ambayo itakuwa inakuingizia kipato kikubwa zaidi. Hapo ndo utaonekana kweli unaelimu. Na wengi wetu tumekuwa na falsafa hiyo na ndicho kitu kinachotukwamisha katika ukuaji wa Elimu na kutufanya tusiwe na maendeleo kabisa. Na ukiangalia wengi wetu tumekuwa tunaridhika mapema, hii ni kutokana na pale mtu anapokuwa ameshaajiriwa na anaweza kupata chochote.
Kwakuwa mtu anakuwa yupo gizani kilemu basi basi hataweza kufanya chochote na Elimu yake itaishia hapo hapo.
Elimu inachocheaje maendeleo ya nchi?
Kama ujuavyo mpenzi msomaji, Elimu ndiyo chachu ya maendeleo ya taifa. Kiongozi akiwa na Elimu ya kutosha atasimamia na kuonesha mwongozo mzuri wa maendeleo na hatakuwa na zile blaa blaa za kisiasa. Mtu mwenye Elimu hufanya kitu(vitu) kwa ustadi na kwakujiamini, kwaasilimia kubwa mtu mwenye elimu hufanya vitu vya uhakika na jamii itamuiga tu.
Je, ni kitu gani kifanyike ili tuweze kujikwamua gizani?
Ili tuweze kujikwamua gizani hakuna zaidi ya kufanya isipokuwa Elimu hiyohiyo ndiyo inayoweza kutupa nuru. Elimu ianzie kwa wazazi kisha irithishwe kwa wahusika au waelimishwaji ili wawe na uchu wa kujifunza zaidi.
Kuwepo na mifano ya kuwahamasisha na hii ni kuanzia kwa viongozi, maana wengi wao wametufanya tuamini kuwa siasa ni inahitaji propaganda ili iweze kuendelea.
Kingine ni kwamba tuwe na wivu Wa maendeleo. Lazima tujiulize kwanini ni watu wa magharibi tu na kwanini isiwe Waafrika ndiyo wakuigwa?
Kwaleo naomba tuishie hapo, nadhani japo kwa uchache lakini tumeweza kupata chochote.

Upvote
3