Pre GE2025 Mwanyemba: Wanaoisaliti CCM ni wanachama wake

Pre GE2025 Mwanyemba: Wanaoisaliti CCM ni wanachama wake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Dodoma , Abdulhabib Mwanyemba amesema wanaokisaliti Chama cha Mapinduzi ni wanachama wake kwa sababu wanafanya makosa wakati wa uteuzi wa wagombea wa ngazi mbalimbali ikiwemo ubunge na udiwani.

Mwanyemba ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake kijijini Kingwe wilayani Bahi mkoani Dodoma ambapo ameongozana na kamati ya utekelezaji ya UVCCM ya mkoa na wilaya.

Amesema wagombea wanaoteuliwa Kupeperusha bendera ya CCM wanakuwa hawakubaliki kwa wananchi na kupelekea kushindwa kipindi cha uchaguzi.

Ziara hiyo imelenga kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuhamasisha wananchi kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao na kuimarisha mashina ya CCM katika wilaya zote za Dodoma
 
Back
Top Bottom