Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Samwel Anthony (34) mkazi wa kijiji cha Shilima wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 8.
Hukumu hiyo imetolewa jana tarehe 20 Novemba 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya wilaya ya Kwimba, Ndeko Dastan Ndeko ambaye ndio Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza mashahidi 5 wa Jamhuri akiwemo mhanga, ambapo Mahakama hiyo imejiridhisha pasi na kuacha shaka kwamba mshtakiwa ametenda kosa hilo
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Juma Kiparo, mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 16 Agosti 2024 huko maeneo ya kijiji cha Shilima, wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza
Mhanga ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kisheria, alifanyiwa kitendo hicho wakati ameagizwa na mama yake dukani na wakati anarudi ndipo mshtakiwa alimvuta nyuma ya nyumba ya baba wa mhanga kisha kumfanyia ukatili huo.
Mshtakiwa alifikishwa mahakamani tarehe 23 Agosti 2024 na kusomewa shtaka la kubaka kinyume na kifungu cha 130 (1)(2)(e) na 131 (3) vya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya Sheria marejeo ya mwaka 2022.
Soma Pia: Afungwa jela maisha kwa kumnajisi mtoto wa miaka 7
Mshtakiwa ameiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa yeye mwenyewe ni mgonjwa wa mapafu, ana watoto watano mmoja mlemavu na pia anamlea mdogo wake ambaye naye ni mgonjwa, na pia mkewe amemuachia mzigo mkubwa wa kulea hiyo familia.
Mshtakiwa licha ya kuomba Mahakama impunguzie adhabu, Hakimu Ndeko amesema kwamba Mahakama hiyo imefungwa mikono kwani kifungu cha 131 (3) cha Kanuni ya Adhabu ambacho mtuhumiwa ameshtakiwanacho kinatoa adhabu ya kifungo cha maisha na hakijampa Hakimu kubadili adhabu hiyo.