Mwanza: Ahukumiwa miaka 30 Jela kwa kubaka mjukuu wake

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mahakama ya Wilaya Sengerema, mkoani Mwanza, imemuhukumu Lucas Maselele (56), mkazi wa kijiji cha Lugata kwenda jela miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mjukuu wake (13) (jina linahifadhiwa) kwa sababu za kisheria.

Hukumu hiyo imesomwa Jana Machi 13, 2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema, Evod Kisoka katika kesi hiyo ya Jinai namba 16492/2024 .

Awali, Mwendesha Mashtaka aliieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni 04, 2024, katika Kijiji cha Lugata, wilaya ya Sengerema kwa kumbaka mjukuu wake wakati mke wake ameenda msibani mpaka alipofumaniwa na mke wake akifanya kitendo hicho kinyume na vifungu vya 130(1)(2)(e) pamoja na kifungu cha 131(1) vya sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya Kwanza tarehe 14/06/2024 baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi na kusomewa shtaka hilo ambapo alikana kutenda kosa hilo.

Upande wa Jamhuri ulileta ushahidi na shauri lilianza kusikilizwa katika mahakama hiyo hadi leo Machi 13 ambapo mshtakiwa alijitetea na kuomba mahakama imuachie huru akidai ni njama tu zilizotengenezwa na mke wake.

Hata hivyo mahakama baada ya kupitia vifungu vya sheria sambamba na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri ikiwemo ripoti ya mganga aliyemfanyia uchunguzi mtoto huyo, mahakama imejiridhisha kuwa upande wa Jamhuri wameweza kuthibitisha shtaka hilo bila ya kuacha shaka lolote kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kumbaka mjukuu wake.
Screenshot 2025-03-14 105032.png
 
Kuweni makini na wanawake nishaswai shudia mmoja akitaka kumpakazia kesui ya aina hiyo mumewe waloachana ila anaish na watoto bahat nzur vipimo vya hospital vilishndwa kuthibisha kubakwa kwa uyo mtoto. Na mtoto alipobamwa na polisi akasema hakubakwa ila mama yake alimwambia aseme ivo
 
Mahakama ya Wilaya Sengerema, mkoani Mwanza, imemuhukumu Lucas Maselele (56), mkazi wa kijiji cha Lugata kwenda jela miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mjukuu wake (13) (jina linahifadhiwa) kwa sababu za kisheria.

Hukumu hiyo imesomwa Jana Machi 13, 2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema, Evod Kisoka katika kesi hiyo ya Jinai namba 16492/2024 .

Awali, Mwendesha Mashtaka aliieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni 04, 2024, katika Kijiji cha Lugata, wilaya ya Sengerema kwa kumbaka mjukuu wake wakati mke wake ameenda msibani mpaka alipofumaniwa na mke wake akifanya kitendo hicho kinyume na vifungu vya 130(1)(2)(e) pamoja na kifungu cha 131(1) vya sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya Kwanza tarehe 14/06/2024 baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi na kusomewa shtaka hilo ambapo alikana kutenda kosa hilo.

Upande wa Jamhuri ulileta ushahidi na shauri lilianza kusikilizwa katika mahakama hiyo hadi leo Machi 13 ambapo mshtakiwa alijitetea na kuomba mahakama imuachie huru akidai ni njama tu zilizotengenezwa na mke wake.

Hata hivyo mahakama baada ya kupitia vifungu vya sheria sambamba na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri ikiwemo ripoti ya mganga aliyemfanyia uchunguzi mtoto huyo, mahakama imejiridhisha kuwa upande wa Jamhuri wameweza kuthibitisha shtaka hilo bila ya kuacha shaka lolote kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kumbaka mjukuu wake.View attachment 3269955
tuache utani mbona ni mwenyewe lucas huyu wa JF .Kamaa yupo kimya mpaka sasa basi ndio tayari
 
Back
Top Bottom