Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Fadhili Nassoro (CCM) ameibuka kidedea wa nafasi ya uenyekiti wa Mtaa wa Calfonia, Kata ya Nyegezi jijini Mwanza kwa kupata kura 1,649 kati ya kura zilizopigwa 2,198.
Akitangaza matokea leo Jumatano Novemba 27, 2024 msimamizi wa uchaguzi, Christer Nyikizeha, amesema waliojiandikisha kupiga kura ni 2,437, waliopiga kura ni 2,266, idadi ya kura halali ni 2,198 na zilizoharibika ni 68.
Soma Pia: MWANZA: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024
Katika matokeo hayo mgombea kupitia Chadema, Yohana Wanga ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 528 na Sauda Ramadhani kutoka SAU akipata kura 22.
Fadhili aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo tangu 2019, alijizolea umaarufu baada ya kupiga magoti kuwaomba msahama wakazi wa mtaa huo Oktoba, 2024 alipokuwa kwenye mkutano wa mwisho wa kukabidhi muhuri wa serikali ya mtaa wake.