Mwanza: Aliyezikwa 2008 kaonekana akiwa hai

Kwani gamboshi (sehemu inayo sadikika kuwa na uchawi mwingi) ipo wapi?
Hiyo Gamboshi ya kichawi hakuna mtu anayeijua ilipo, ni kama tunavyosadikishwa akhera.

Ukiulizwa, mbinguni ni wapi, hauwezi sema dhahiri upande ilipo mbinguni kwa ufanisi bali kwa hisia za kiimani.

Gamboshi ni jina la kijiji kinachopatikana Bariadi vijijini, ni kijiji cha kawaida kabisa watu wakiendelea na shughuli zao na hakuna masuala hayo kiurasmi na kama yapo, basi ni kama yalivyo katika maeneo mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo nimekupata Maana wengi wanajua gamboshi ni Moja tu ambako ndipo eneo ambalo watu wanaishi kawaida na eneo hilo hilo ambako nadharia ya uchawi ilipo.
 
Wewe bora unyamaze na kauli yako iishie hapo hapo .Hakuna uchawi unaotegemewa usukumani kama huo, na ni mwingi sana , ndugu acha kabisa, wakikutaka hawakukosi, ukiona mtu ametokezea baada ya kuzikwa, basi ujue aliyewachukua kafariki, usiombe kushuhudia ndugu, utalia kwa uchungu, namna wanavyoteseka!! mimi nilishuhudia kwa macho na niliponea bahati tu. Acha kabisa.
 
Huyu mama kwao ni magu, ila alikuwa ameolewa maeneo ya wilaya Ma$wa . Nilienda kumuona wakati ameonekana. Kweli alikuwa amekufa, na alizikwa kwao wilayani magu kijiji cha n'haya. Na kuna waliokufa alikuwa nao kule aliko kuwa aliwataja majina, ila wao hawajaonekana.
 
Hivi vitu kama haujajionea unaweza zani maigizo kua havipo kwamba ni usanii tu.

Ila Binafsi naamini haya mambo na natamani kukutana na mtu aliye patwa na kisanga hicho walau nifanye nae mahojiano.
 
Kumbaff. Tuko nyuma vipi wakati ni sayansi ya kawaida huko kwetu ushashini?
 
Jambo kama hili liliwahi pia ripotiwa na ITV, kama sikosei ilikuwa 2008 /2009, ila tukio lilitokea moshi. Hadi magazeti yaliandika. Haya mambo yapo sana tu. Ushirikina
 
Hivi vitu kama haujajionea unaweza zani maigizo kua havipo kwamba ni usanii tu.

Ila Binafsi naamini haya mambo na natamani kukutana na mtu aliye patwa na kisanga hicho walau nifanye nae mahojiano.
Miaka ya 1990s mzee wangu aliwahi kuwa ocd wilaya hiyo ya bariadi kilichopo hicho kijiji cha gamboshi, akikusimulia matukio yaliyokua yanatokea kwenye hicho kijiji unaweza ukashangaa.
 
Sasa umeandika nini mkuu? Point yako ni ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…